Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Dk Mwinyi atoa maagizo mawaziri wapya

9115e5c9346c8114770f6daf821937db Dk Mwinyi atoa maagizo mawaziri wapya

Sat, 21 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi leo amewaapisha mawaziri 15 ambapo amewataka kuwa na hati nne kwa ajili ya kuengeneza mpango kazi kwa ajili ya wizara zao katika kipindi cha miaka mitano ikiwemo kufahamu vizuri muundo wa wizara na taasisi zote zilizopo chini yake.

Akizungumza katika hotuba yake Ikulu Zanzibar, Dk Mwinyi aliwashukuru mawaziri wote kwa kukubali uteuzi huo na kubainisha kuwa hakuna aliyemtaarifu juu ya uteuzi wake.

Hati ambazo mawaziri hao wanatakiwa kuwa nazo ili kutengeneza mpango kazi katika wizara zao kwa kipindi cha miaka mitano ni kama ifuatavyo;

1.Ilani ya uchaguzi inasema nini katika wizara

2.Hotuba aliyotoa katika Baraza la Wawakilishi inaelekeza nini kwenye wizara

3.Ahadi kipindi cha kampeni zinasemaje

4.Kupata maoni ya wadau kuhusu wizara

Katika hatua nyingine Dk Mwinyi amewataka mawaziri waliokula kiapo kuwajibika ipasavyo na kuhakikisha kila mtumishi anatekeleza wajibu wake kwa wananchi.

Columnist: habarileo.co.tz