Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

DK MWINYI AJA NA MUAROBAINI KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYA BIASHARA

Capture 533?fit=437%2C343 DK MWINYI AJA NA MUAROBAINI KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYA BIASHARA

Sat, 5 Dec 2020 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa Serikali anayoiongoza itatoa msukumo mpya katika kutatua changamoto zinazokabili biashara hapa Zanzibar.

Rais Dk. Hussein Mwinyi aliyasema hayo leo katika hotuba yake aliyoitoa katika mazungumzo kati yake na wafanyabiashara wa Zanzibar, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil, Kikwajuni Jijini Zanzibar.

Katika hotuba yake Rais Dk. Hussein Mwinyi alisema kuwa anataka kuweka mashirikiano na sekta binafsi pamoja na kuongeza na kuwepo mijadala ya wazi na yenye tija kwa lengo la kuweka mazingira mazuri kwa wafanyabiashara.

Rais Dk. Hussein alisema kuwa Serikali haifanyi biashara bali kazi yake ni kutengeneza Sera nzuri, sheria, kanuni, na kuweka mifumo ya udhibiti wa biashara lakini uchumi utaendeshwa na sekta binafsi.

Aliongeza kuwa Serikali itaweka mfumo rafiki, kuondoa urasimu, rushwa na vikwazo vyote vinavyotakana na utendaji mbovu.

Rais Dk. Hussein alieleza maono yake ni kuifanya Zanzibar kuwa ni kituo cha biashara katika Afrika Mashariki hasa kutokana na mazingira yake kijiografia kwani Zanzibar inaweza ikawa kituo cha biashara, utalii, viwanda, bandari huru hiyo ni kutokana na jinsi ilivyo.

Rais Dk. Hussein alirejea kauli yake ya kuwataka viongozi wa Mawizara kutengeneza mipango yenye bajeti huku akisema kuwa kila sekta ina utaratibu wake na kwa upande wa ujenzi wa barabara Serikali itafanya na kuchukua jukumu lake hilo la kujenga barabara na sio sekta binafsi.

Alisema kuwa madhumuni ya mkutano huo ni kutimiza ahadi yake aliyoahidi wakati wa Kampeni ya kukutana na wafanyabiashara na kutaka kujua changamoto zao na kuahidi pale atakapaingia madarakani watakaa pamoja huku akieleza kwamba changamoto zote amezisikia na zitafanyiwa kazi hasa ikizingatiwa viongozi wa Serikali walikuwepo katika mazungumzo hayon wakiwemo Mawaziri na Makatibu Wakuu.

Katika maelezo yake alisema kwamba zipo tabia ya kufanya mikutano mingi bila ya ufumbuzi ambapo katika utawala wake tabia hiyo hatoitaka na kusisitiza kwamba kuchukuliwa changamoto na kutofanyiwa kazi ni kupoteza muda hivyo ni lazima mikutano iwe na tija.

Hivyo, aliwaeleza watendaji wote Serikalini kwamba ana miadi na wananchi katika miaka mitano hivyo ni lazima kufanya kazi kwa haraka ili kutatua changamoto zilizopo na kama zikitokezea kuwashinda apalekewe.

Alisema kuwa kwa upande wa bandari, katika mradi huo kuna uwezekano mkubwa wa kushirikiana na sekta binafsi.

Columnist: zanzibar24.co.tz