Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

DIAMOND PLATNUMZ, Apewe kura za ndio tuzo za BET

3d3537eecb122a24e8ff95c021ec8d2e.jpeg DIAMOND PLATNUMZ, Apewe kura za ndio tuzo za BET

Sat, 5 Jun 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

DIAMOND Platnumz ndiye mwamuziki pekee kutoka Afrika Mashariki anayewania tuzo za BET kwa mwaka huu.

Ni hatua kubwa kwa Diamond kuwemo katika kinyang’anyiro cha kuwania tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Kimataifa katika tuzo hizo za BET.

Diamond katika mbio hizo za kusaka tuzo hiyo atachuana na wakali wengine na nchi wanazotoka zikiwa katika mabano kama akina Aya Nakamura (Ufaransa), Burna Boy (Nigeria), Emicida (Brazil), Headie One (Uingereza), Wizkid (Nigeria), Young T & Bugsey (Uingereza) na Youssoupha (Ufaransa)

Hii sio mara ya kwanza kwa Tanzania kuwa na msanii anayewania tuzo ya BET, ambapo mwaka 2017, Rayvanny alishiriki na kuwa Mtanzania wa kwanza kushinda tuzo za BET.

Na hii ilimfanya Rayvanny kuwa msanii wa pili Afrika Mashariki kushinda tuzo ya BET baada ya Eddy Kenzo aliyeshinda tuzo ya msanii mwenye watazamaji wengi kimataifa mwaka 2015.

Mbio hizo za kuanza kusaka tuzo hiyo pamoja na zingine za BET zinatarajia kuanza Juni 7, ambapo kura zitaanza kupigwa huku shindano mshindi akitarajiwa kutangazwa Juni 27, na kuoneshwa mubashara.

DIAMOND PLATNUMZ

Tangu alipotangazwa, mwanamuziki, Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuwania tuzo maarufu duniani za BET katika kinyanyiro cha mwanamuziki bora wa Kimataifa, kumeibuka makundi mawili, linalotaka aungwe mkono na jingine linapinga.

Wapo ambao wamechukulia ushindani huo ni kama ule wa Simba na Yanga au wa vyma vya kisiasa, kwamba atakayeshinda atajipatia sifa yeye na kundi lake, hivyo mpinzani anakuwa hataki mwenzake ashinde.

Kama ilivyokuwa kwenye mpira huenda shabiki wa upande mmoja asiwe na faida yoyote kwa upande ambao utashinda, au upande ambao utashindwa lakini kwake ni kuona anapata burudani ya muda mfupi bila ya kujalli faida inayoweza kuletwa na ushindi wa mpinzani wake.

Labda tujiulize kwanini wasanii wengi wameungana kutaka Diamond Platnumz ashinde tuzo ya BET wananufaika na nini na taifa linanufaikaje na kwanini wapo ambao hawataki ashinde.

Tuzo za BET ni ndoto za karibu wanamuziki wote Duniani, ndio maana mwanamuziki anapokosa au kushindwa kuchaguliwa kuwania tuzo hizo

Analalamika sana kwakuwa wanaamini wanatakiwa kutunukiwa heshima .

Tuzo hizo zilianza rasmi mwaka 2001 nchini Marekani zikiwa na vipengele mbalimbali, na kutoa tuzo kwa wasanii wakubwa duniani akiwemo Chris Brown, Dj Khalid, Whitney Houston na wengine wengi.

Wasanii hasa wa Afrika kuchaguliwa katika tuzo hiyo ni ufahari mkubwa haijalishi ameshinda au amekosa, lakini jina lake kuwepo pale ni kigezo kwamba anafanya vizuri.

Katika muziki wa nchi za Afrika imekuwa sehemu ya kipimo kwamba mwanamuziki unasogea na kutambulika kimataifa zaidi, kwakuwa nchi inajitangaza katika tasnia ya muziki na utalii kwa kufuatiliwa zaidi.

Hakuna taifa lililokosa migogoro ya ndani kati ya msanii na msanii, lakini linapokuja suala la fursa ya kitaifa hasa katika tuzo kubwa kama hiyo, wasanii wote wanatakiwa kuungana.

Hii pia kwa Tanzania robo tatu ya wasanii wakongwe na wachanga wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha Diamond Platnumz anafungua milango ya ukombozi wa muziki wa Bongo Fleva kwa kuleta tuzo hiyo nyumbani.

Karibu kila msanii ameandika lake kumuombea kura mkongwe huyo, akiwemo Mbunge wa Muheza na mwanamuziki Hamisi Mwijuma ‘ Mwana Fa’ ambaye katika kurasa yake ya Instagram ameandika:

Muziki wa Tanzania unatokea sababu ya juhudi kubwa za wasanii wenyewe na wadau wengine kwenye sanaa hiyo, matokeo ya namna hii yana usherehesha na ndio nyakati tunafaa kuwabeba watu wetu na kutusogeza wote mbele na karibu na Ufalme wa Muziki duniani.

“Kuwania BET sio jambo dogo, na niwaombe tufanye linalotakiwa kufanywa kumuwezesha kijana wetu Diamond Plantumz kurudi na hii tuzo nyumbani” anaandika.

Mwana Fa amegundua kwamba kushinda kwa Diamond katika tuzo hizo, sio manufaa kwa mwanamuziki huyo ila ni faida kwa taifa zima, kwani muziki wetu utasogea mbele kimataifa.

Nickson Simon ‘Nikki wa pili’ ni mwanamuziki anayeaminika kuwa ni miongoni mwa wanamuziki wasomi na wenye uelewa mkubwa, hasa katika kutetea haki za wasanii, asiyeogopa kuongea ukweli anasema Tanzania kama nchi na Bongo Fleva kama kiwanda bado tuna njaa kubwa sana ya tuzo za nje.

“Lini tumeshiba mpaka tuanze kubeza kushinda tuzo ni njaa tu hiyo, tukishiba tuzo tutakuwa na malumbano ya nani alete nyingi zaidi, ila sasa ni njaa ya tuzo inatusumbua na dawa yake nikushinda nyingi zaidi.”

Nikki alifafanua zaidi kwamba tuzo inapokuja haiji peke yake inakuja na watu kuitazama Tanzania, wafanyabiashara kutugeukia, viwanda vingine kutaka zaidi kuungana na sisi.

Kuna ambao pia kwa kuandika mambo ya wasanii kwa ubaya au uzuri ndio mnapata followers na mnapata biashara, kifupi mnadeni kubwa kwa wasanii, wapigieni kampeni wakiibuka na nyie mnaibuka.

Niki anaamini kwamba tuzo ya BET haiji na Diamond pekee, ila inakuja na wawekezaji katika muziki wa kizazi kipya, huenda hata mataifa ya nje yakaja kutafuta fursa kutokana na ushindi wa Diamond.

Kuonesha kwamba tuzo hizo zinatizamwa zaidi kwa macho mawili, mfanyabiashara mkubwa Afrika na muwekezaji katika timu ya Simba SC, Mohamed Dewji anasema kuteuliwa kwa Diamond katika tuzo za BET, ni kujivunia kwakuwa anaamini anaiwakilisha nchi.

Mo Dewji angeweza kukaa kimya kwakuwa hausikii, lakini kwakuwa ni mfanyabiashara anaamini kwenye biashara anaamini kwamba Diamond anaweza kuja na biashara mpya kupitia muziki .

Tabia ya mfanyabiashara kutochagua biashara yenye hasara, hivyo ipo siku tukasikia amewekeza fedha nyingi kwenye muziki baada ya muziki kuonekana umetanuka zaidi, hasa katika mataifa makubwa ya Afrika na duniani kwa ujumla.

Japo kuna matarajio hayo ya wengi wakihitaji tuzo hiyo ije Tanzania, lakini lipo kundi ambalo wanaamini Tanzania haistahili kupata hiyo tuzo kupitia Diamond Platnumz.

Katika kundi hilo wapo ambao wamekuwa wakileta mhemko wa kisiasa, wengine chuki binafsi na hata chuki, huku lipo kundi linaamini litapata umaarufu kwa kujiunga na kundi la wapingaji.

Wanaochukulia kisiasa wanashindwa kuelewa kama wao wanashabikia upande fulani wa siasa, lazima watakuwa wanamanufaa yao, ndivyo hivyo Mtanzania yoyote anahaki ya kushabikia upande wa siasa na sio arushiwe hilo jiwe.

Harafu Diamond sio mgombea wa chama chochote, huenda katika kutafuta maslahi mapana ya kampuni yake na hayo yalifanywa hata na wanamuziki wakubwa akiwemo Kanye West, Jay Z, Michael Jackson lakini haikuondoa uzalendo wao katika nchi yao.

Wengine wanadai kwanini haweki picha ya mtu kwenye akaunti yake, na kushindwa kuelewa kwa ndani ya nchi kila msanii anavutia kwake na kundi lake kwaajili ya chakula chake, lakini kwa kimataifa lazima uvutie taifa lako kwanza.

Kuna watu wao wanatafuta umaarufu kwenye mitandao ya kijamii, sio mameneja sio wasanii, ila wanafanya mradi waonekane wamefanya kwa maana muziki ufe au usife kwani wao hawana faida yoyote.

Hata wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameitisha wito wakitaka msanii huyo apigiwe kura ilia pate tuzo hiyo.

Yoye na yote kikubwa tumpigie kura Diamond Platnumz ili alete tuzo nyumbani, baada ya tuzo kurudi tuanze na mabifu yetu ya ndani ili kesho muziki uje na ajira mpya.

Columnist: www.habarileo.co.tz