Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Cyprian Musiba atangaza kumshitaki Tundu Lissu

1337 Musiba 624x400 TZW

Tue, 16 Jan 2018 Chanzo: millardayo.com

Mkurugenzi wa Kampuni ya CZI, Cyprian Musiba leo January 15, 2018 amezungumza na waandishi wa habari na kueleza kuwa yeye na baadhi ya Wanasheria nchini katika siku mbili zijazo watamfungulia mashtaka Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu.

Ameeleza kuwa wamefikia uamuzi huo kutokana na maneno aliyoyatoa Lissu kabla ya kwenda nchini Ubelgiji kwaajili ya matibabu, kwa kutoa kauli nzito kuwa Tanzania kwasasa sio mahali salama pa kuishi na eneo hatarishi kwa maisha ya binadamu.

Musiba ameeleza kuwa kauli hizo zililenga kuidhalilisha nchi, kuwapa hofu wageni wanaokuja nchini kwa ajili ya kutalii lakini pia kuwaogopesha wananchi washindwe kufanya kazi zao kwa amani na hivyo wanahitaji aisaidie nchi kutoa uthibitisho wa kauli zake hizo katika vyombo vya sheria.

“Tunampa siku mbili atoe uthibitisho wa kauli zake vinginevyo tutampeleka mahakamani, na japokuwa tutampeleka katika mahakama za ndani, nakala yake itapelekwa The Hague Uholanzi kwenye Mahakama ya Kimataifa.” – Cyprian Musiba

Kamanda Kikosi cha Usalama Barabarani alivyokutana na Traffic katika eneo hatari kwa ajali



HEKAHEKA: Mwendelezo Kichanga cha miezi miwili kilichopotea kimepatikana kiutata

Columnist: millardayo.com