Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Corona yawaumiza vichwa wafanyabiashara mtumba Mwenge

CORONA Corona yawaumiza vichwa wafanyabiashara mtumba Mwenge

Wed, 17 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

“DUH!, hii corona sasa inakoelekea itatulaza na njaa” Rama alijikuta akiropoka kwa sauti , huku akiikodolea macho simu yake katika mtazamo wa kutoamini anachokiona.

“Kuna nini tena” aliuliza jirani yake huku akielekea aliokuwapo Rama ili na yeye aone kinachomsibu.Kama ilivyotokea kwa Rama naye alitahamaki, “kweli aisee kwa hali hii tutafunga biashara”.

Kwa ya dakika kadhaa hali ya taharuki ilitawala katika soko la mitumba Mwenge, makundi ya watu yalionekana wakijadili jambo , ujumbe unaosambaa kwenye whatsap’ uliwafungulia mada ya mwenendo wa biashara yao.

Ni ujumbe wa njia ya sauti unaotahadharisha watu kutonunua nguo za mtumba kwa kipindi hichi cha mlipuko wa corona kwa kuwa kuna mabelo ya nguo za mtumba walizotumia wagonjwa wa corona nchini China yataletwa nchi za Africa.

Ramadhani Mikidadi, maarufu kama Rama, ni mfanyabiashara wa bidhaa za mtumba ya midoli yaa watoto ya sokoni hapo, anayesema tangu kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa wa corona mauzo yameshuka kutokana na mzunguko kuwa mdogo lakini anahofu ujumbe huu unaozunguka unaweza kuua kabisa biashara yake.

“Ujumbe huu umenishtua kwa kuwa mimi nategemea wateja wa nguo za mtumba ndio wanunue na kwangu, sasa kutokana na huu ujumbe kutembea ni dhahili kuwa wateja wa nguo za mtumba hawatokuja tena huku”, anasema Rama

Tangu kuenea kwa ugonjwa wa corona Rama analalamika biashara yake kudodora kutokana kukosekana kwa wateja ambao wanakaa ndani kuepuka msongamano.

“Biashara imeyumba sana dada, zamani nilikuwa nikikusanya hadi Sh. 100,000 kwa siku ila kwa sasa nikipata sana ni Sh. 10000, hii yote ni kwa sababu mzunguko wa watu umepungua”, analalamika Rama.

Naye mfanyabiashara wa nguo za mtumba, Obo anasema biashara ya nguo za mtumba imeshuka kwa sababu,watu hawavutiwi kununua nguo za mtumba kwa kuwa hakuna tena shughuli za kumlazimu mtu kununua nguo.

“Unajua nguo za mtumba zinaendana na ‘occasion’ (shughuli maalum)”,ambayo kwa sasa serikali imezuia ili kupisha hili gonjwa la corona, kwa hiyo watu hawana sababu ya kuja kununua nguo.

Obi ambaye kabla ya kuzuka kwa ugonjwa wa corona alikuwa akiuza kati ya Sh. 65000 hadi 100,000 kwa siku, kwa sasa anapata Sh. 20,000 kwa siku, analalama kuwa kama ujumbe huu ukiendelea kusambaa anaweza asiuze kabisa kwa siku.

Japo idadi kubwa ya wafanyabiashara wanalalamika kudorora kwa mauzo, kwa uande wa pili wa shilingi, wapo ambao hawajaathirika sana.

Grace maiko, mfanyabiashara wa pochi na viatu vya mtumba, anasema kwa upande wake biashara si mbaya kwa sababu hategemei sana wafanyabiashara wa kupita bali wa mtandaoni.

“Mimi bidhaa zangu nauza sana mtandaoni ndugu mwandishi, hapa nimeegesha tu, bidhaa zangu napiga picha, naweka insta, mteja akipenda, analipia nampa bodaboda anampelekea alipo” anasema Grace kwa kujiamini.

Zuberi Kafumula hatofautiani sana na Grace, ingawa yeye ana banda la biashara katika eneo hilo, lakini amejikita zaidi kuuza bidhaa kwenye minada, kwa hivyo mauzo yake hayajashuka.

Tangu wahamishiwe katika soko jipya, wateja walikuwa hakuna hivyo alijiongeza na kuwa anakwenda kuuza bidhaa zake kwenye minada na kujikuta hategemei sana kuuza biashara zake katika soko hilo.

WENGINE WAKIMBIA

Hali ngumu ya mauzo katika soko hilo kipindi hichi cha mlipuko, kimewalazimu wafanyabiashara wengine kukimbia eneo hilo wengine kuacha kwa muda, kutafuita biashara sehemu nyingine wakiamini huko kuna nafuu.

Ismaili amelazimika kuhama eneo la biashara la mwenge na kwenda tandika kujishkiza na anasema atarudi baadaye pindi biashara itakapochangamka kama zamani.

“Ujajua tangu tuhamie soko jipya biashara ni ngumu kutokana na kwamba wateja wengi hawajakuzoea huku, sasa tangu kweo huu mlipuko hali imekuwa mbaya zaidi” anasema ismaili na kuongeza

“Sikufichi dada yangu ilifika mahali nikawa sipati hata shilingi wiki nzima, nikaona nijiongeze kutafuta sehemu iliyochangamka ili niokote okote, nitarudi hali ikikaa sawa “.

Wakati wengine wakihama, baadhi ya wafanyabiashara wenye biashara zaidi ya moja, wamelazimika kufunga biashara sizizo na wateja ili kupunguza hasara.

Dominiki , maarufu kama domy , aliyekuwa na biashara mbili amelazimika kufunga biashara ya kuuza midoli na kubaki na biashara ya kuuza viatu kwa kuwa ndio inawateja kwa sasa.

HALI ILIVYO

Kulingana na taarifa ya Wizara ya afya kuhusu Ugonjwa wa virusi vya corona nchini Tanzania, idadi ya watu waliothibitika kuwa na maambukizi ya ugomjwa huo mpaka sasa wamefikia 32, huku wagonjwa 3 wakifariki dunia, na watano kupona kabisa.

“Hivyo sasa, jumla ya watu waliothibitishwa kupata maambukizi ya Covid 19 nchini ni 32, kati ya hawa watano wamepona na wengine 24 wanaendelea vizuri na matibabu”, alisema Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakati akitoa taarifa hiyo.

Kwa upande mwingine, hali ikiwa mbaya zaidi nchini marekani kwa kuweka rekodi ya kuwa na zaidi ya vifo 2000 vya virusi vya corona kwa siku moja.

Takwimu kutoka Chuo Kikuu Johns Hopkins zinaonyesha kuwa watu 2,108 wamekufa katika kipindi cha saa 24, huku kukiwa sasa na zaidi ya watu nusu milioni walioambukia virusi hivyo nchini Marekani.

Katika kujikinga na maabukizi ya virusi hivi vinavyoenea kwa kasi kwa njia ya hewa na kushikana Serikali imezuia mikusanyiko yote ya watu wengi yakiwemo matamasha ya muziki, mikutano ya hadhara mbalimbali ikiwemo ya kisiasa.

Vilevile imekua ikiwahamasisha watu kunawa mikono na kutumia vitakasa mikono ili kuepuka kuambukizwa au kusambaza virusi vya hivyo.

Columnist: www.tanzaniaweb.live