Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Changamoto zilizoibuliwa na CAG zifanyiwe kazi

Bcc69dc078d46d00af6362df7249c1b4.jpeg Changamoto zilizoibuliwa na CAG zifanyiwe kazi

Fri, 9 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

JANA Ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ziliwasilishwa bungeni na mawaziri wa sekta husika na baadaye CAG, Charles Kichere alizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kutolea ufafanuzi hoja zilizobainika katika ripoti hizo za mwaka wa fedha 2019/2020.

Baadhi ya ripoti zilizowasilishwa bungeni ni Ripoti Kuu ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu Ukaguzi wa Taarifa za Fedha za Serikali Kuu kwa Mwaka wa Fedha ulioshia Juni 30, 2020; Ripoti Kuu ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu Ukaguzi wa Taarifa za Fedha za Miradi ya Maendeleo kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Juni 30, 2020 na Ripoti Kuu ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu Ukafuzi wa Taarifa za Fedha za Mashirika ya Umma kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Juni 30, 2020.

Nyingine ni Ripoti ya jumla ya Ukaguzi wa Ufanisi na Ukaguzi Maalumu kwa kipindi kilichoishia Machi 31, 2021;

Ripoti Kuu ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu Ukaguzi wa Taarifa ya Fedha za Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha ulioshia Juni 30, 2020.

Pia ziliwasilishwa Taarifa ya Majibu ya Serikali na Mpango Kazi wa Utekelezaji wa Mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Hesabu za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa Mwaka ulioshia Juni 30, 2020 na Majumuisho ya Majibu na Hoja na Mpango wa Kutekeleza Mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Hesabu za Serikali Kuu na Mashirika ya Umma kwa Mwaka wa Fedha ulioshia Juni 30, 2020.

Kwa mujibu wa CAG Kichere, ripoti hizo na nyingine zilizowasilishwa bungeni, zimeonesha kuna hoja nyingi zilizoibua changamoto za ukiukwaji wa taratibu za hesabu za serikali kwa watu waliopewa dhamana ya kuzisimamia.

Kutokana na hilo, CAG ameonesha kuwapo kwa kasoro nyingi katika hesabu hizo kiasi cha kuzaa ukiukwaji mkubwa wa taratibu na matumizi ya fedha za umma ambayo hayana maelezo yakinifu ya matumizi hayo na hivyo fedha za serikali kutumika isivyo sawa.

Tunafahamu kuwa wabunge na serikali kwa upande wake itakuwa na majibu ya hoja za CAG, ni vyema kukawepo na msukumo wa kusisitiza kwa wahusika kuhakikisha hali hii haiendelei kwa sababu inapoteza fedha za umma na hivyo itasababisha kuzorota kwa utoaji huduma kwa wananchi.

Ni imani yetu serikali itachukua hatua za kudhibiti hali hii kwa kuwachukulia hatua watendaji ambao itabainika wamekwenda kinyume cha taratibu na kusababisha hoja zilizotolewa na CAG, lakini pia itachukua hatua za kuhakikisha changamoto hizi zinapungua kama siyo kwisha kabisa katika mwaka unaofuata.

Columnist: www.habarileo.co.tz