Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Chama Atakuwa Okwi Mpya Simba?

Chamaa Chama Chama amerejea Simba kwa mara nyingine baada ya kuuzwa Morocco mwaka jana

Sat, 15 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ni swali ambalo pengine unaweza ukawa unawaza na kujiuliza kama mimi juu ya Mwamba wa Lusaka Clatous Chota Chama kama ‘Je, ni atakuwa Okwi mpya Simba?

Kwanini nawaza kurudi kwa Chama na kumrandanisha na mshambuliaji kutoka Uganda Emmanuel Arnold Okwi ambaye alikuwa mfalme wa Simba Sc?

Kihistoria, Mshambuliaji kutokea Uganda Emmanuel Okwi aliwahi kukichapa pale Msimbazi kwa misimu mitatu tofauti tofauti ingawa alianza kuvaa jezi ya Simba akiwa bado kijana mdogo.

Emmanuel Arnod Okwi alijiunga na klabu ya Simba kwa mara ya kwanza mwaka 2010 akitokea klabu ya Sc Villa na kukiwasha klabuni hapo hadi mwaka 2013 akiwa kama kiungo mshambuliaji.

Umahili na jina lake halikutoka midomoni mwa wanasimba hii ni kutokana na uwezo wake wa kuzisalimia nyavu za mpinzani, uwezo wa kuisumbua timu pinzani lakini kubwa aliteka mioyo ya Wanasimba.

Zile mbwembwe zake na umahili wake hatukuuona tena kwenye msimu wa mwaka ‪2013-2014‬ baada ya klabu ya Simba kumuuza kwa dolla 300000 kwenda kuitumikia timu ya Etoile du Sahel.

Labda niseme Simba ilihitaji sana huduma yake lakini kwenye klabu ya Etoile du Sahel hakupata nafasi kama Msimbazi, vijana wanasema kiwango kilishuka ghafura ikichagizwa na mambo mbalimbali kama vyakula na mazingira.

Msimu wa ‪2014-2015‬ Okwi alirudi tena Msimbazi. Ni ukweli usiofichika Emmanuel Okwi alijizolea umaarufu siyo labda kwa kuwa Simba ina mashabiki wengi la hasha! ni kwasababu ya kazi yake mzuri ya kupachika mabao. Kitakwimu aliweka kimiani mabao 16 kwenye mechi 20 alizocheza.

Licha ya ubora huo, Simba iliachana na mshambuliaji huyo na kupotea kwenye macho ya wanamsimbazi kwa msimu wa mwaka ‪2015-2016‬ alipokua akikiwasha katika timu ya Sc Villa Kabla ya kurudi tena msimbazi msimu wa ‪2017-2019‬

Katika msimu wake wa mwisho Okwi alihusika kwenye jumla ya magoli 53 huku akiweka kimiani magoli 36.

Ikumbukwe kuwa, Msimu wa ‪2015-2016‬ Emmanuel Okwi hakupata kabisa nafasi ya kukiwasha katika klabu yake ya Sc Villa kwa maana nyepesi Okwi alifulia.

Hapa ndipo napopata swali la kujiuliza ‘je, Chama ni Okwi mpya?’ Kwa sababu tangia mshambuliaji huyo kutoka klabu ya Simba na kujiunga na RS Berkane hajawa kwenye kiwango ambacho wanasimba na wepenzi wa soka walikishuhudia.

Labda pengine RS Berkane kuna wakali zaidi yake lakini bado nabaki njia panda, je kiwango chake kitakuwa kama ilivyokuwa kwa Emmanuel Okwi ambaye alikuwa anatoka akiwa moto na kujikuta akipokea ghafura kabla ya kurudi Tanzania na kurudisha utawala na enzi.

Okwi anaoneka kutokuwa kwenye fomu kwenye klabu zingine lakini aliporudi Simba alikiwasha. ‘ je, Chama ni Okwi mpya Simba?

Columnist: www.tanzaniaweb.live