Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

CHINI YA KAPETI: Juni Calafat, binadamu nyuma ya Real Madrid

Fede Valverde Ggg Federico Valverde

Mon, 30 Jan 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Septemba 11, 2022 ilikuwa Jumapili katika mechi ya La Liga baina ya wenyeji Real Madrid dhidi ya Real Mallorca iliyomalizika kwa Los Blanco kushinda mabao 4-1 yaliyofungwa na Federico Valverde, Vinicius Jr, Rodrygo na Antonio Rudiger na lile la wageni likifungwa na Vedat Muriqi.

Jioni ya siku hiyo Real Madrid ilicheza kama watoto wa baba mmoja aitwaye Juni Calafat. Msingi nyuma ya nyumba ile nzuri, ni nguzo nyuma ya ukuta ule imara.

Ni nani huyu Juni Calafat? Ni ukamilisho wa pembe tatu ndani ya Real Madrid. Utamtaja Rais Florentino Perez, kisha mtu wake wa karibu, Jose Angel Sanchez lakini bado utapaswa kumaliza na jina la Juni Calafat.

Ndiye mhimili wa vipaji vingi vya Madrid kutoka Amerika Kusini hata kama vimejificha Montevideo, Uruguay au Buenos Aires, Argentina ama Sao Paulo huko Brazil, watavifikia na vitacheza Bernabeu.

Wengi hupenda kuhusisha mpira na wachezaji waliocheza kwa mafanikio makubwa, lakini dunia hivi sasa inapokea majina kama Jose Mourinho, Luis Campos na kina Calafat ambao hawakucheza kwa mafanikio makubwa, lakini wameutendea mpira wa miguu makubwa sana.

Ndiye kichwa nyuma ya hii Real Madrid japo hakuwahi kuwa mchezaji mkubwa.

Calafat alianza kuingia kwenye mpira kama mtu wa karibu na Ronaldo De Lima wakati huo anakipiga Real Madrid na ndipo hapo taratibu akatengeneza kuaminika na kuanza kukubaliwa na nyota wengi wa Brazil sambamba na familia zao. Taratibu kupitia kazi zake bora akajipenyeza rasmi ndani ya Real Madrid 2013 ambapo alikuwa na mahaba mazito na soka la vijana.

Mpaka sasa ndiye skauti mkuu wa timu hiyo huku akiunda timu kubwa ya ushindi duniani kote ambayo ina macho kama tai kwenye suala la kusaka vipaji duniani.

Mzaliwa huyo wa Hispania ndani ya Jiji la Madrid akifahamika kama Jose Antonio Calafat de Souz mwaka 1972 wakati huo Tanzania ikiwa bado nchi ya ujamaa, makuzi yake makubwa ni nchini Brazil na ndipo alipofahamu mengi kuhusu soka na wachezaji wengi wa Amerika Kusini.

Nyuma ya usajili wa Vinicius Jr na Rodrygo, Eder Militao ni yeye huku pia alimtambua nyota kama Matthjs De Ligt angali mdogo kuwa ni mmoja kati ya wachezajj bora wajao kutoka Ulaya. Bahati mbaya Real Madrid hawakumsaini. Ikumbukwe pia mpango binafsi wa Rais Perez ni kutokubali wamkose Neymar mwingine kutoka Brazil akafanya kila ajuacho ili kipaji halisi kutoka nchi hiyo kicheze Real Madrid

Mpaka sasa moja kati ya saini zake bora ni Fede Valverde kutoka Uruguay, Adry Lunin kutoka Ukraine, Martin Odegaard, Edu Camavinga na Aurelien Tchouameni ambao hawatokei Brazil alipo na mizizi zaidi. Hii ni sawa na kusema samaki wake wazuri zaidi amewavua kwenye bahari tofauti na Brazil. Bado anaendelea kuonyesha uwezo. Kuna wakati anafeli lakini mara nyingi amefaulu vyema.

Columnist: Mwanaspoti