Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Bora kuangalia hotuba ya mama

Hotuba Pic Data Bora kuangalia hotuba ya mama

Fri, 14 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

KWA zaidi ya miaka 10, wikiendi iliyopita ndio ilikuwa wikiendi yenye kumbukumbu mbaya zaidi kwa mashabiki wa Simba na Yanga na wadau wa soka la Tanzania baada ya mchezo baina ya wababe hao kuahirishwa.

Wazee wa vibanda umiza tulikusanya ripoti za matukio kutoka sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam na hapa tunakosegezea nini kilijiri wakati mchezo huo ulipochelewa kuanza na baadae kuahirishwa kabisa.

Hii imetokea maeneo ya Yombo Kilakala shabiki mmoja mkubwa wa Simba alishuhudia mechi akiwa huko.

Jamaa anasema kulikuwa na matukio mawili makubwa, tukio la kwanza ilikuwa ni wakati mchezo unachelewa kuanza na basi la Yanga kuonekana likitoka uwanjani.

Baadhi ya mashabiki walioonekana kuisubiri derby kwa hamu walianza kumlazimisha mmiliki wa banda aweke hotuba ya Rais Samia Suluhu Hassan, maana kilichoendelea kiliwatia kichefuchefu.

“Oya weee, tutolee huo utumbo hapo, mbele bora uweke hotuba ya Mama tu, tuangalie. Mimi kila siku nawaambia TFF na viongozi wake ni watu wa matumbo tu hawana lolote.”

“Wewe umeongea jambo la maana bora itolewe tu, tuangalie mambo ya maana, huu utumbo unakera.

Kiasi cha nusu la banda kiliafiki iwekwe hotuba, lakini kuna wengine hawakupenda jambo hilo ikiwamo jamaa mmoja aliyevaa jezi ya Simba.

Baada tu ya kubadilishwa, jamaa hakuongea sana zaidi ya kunyanyuka na kusogea karibu na soketi iliyokuwa karibu na mlango wa kutokea kisha akazima, akageukia watazamaji, akatukana na kuchomoka kama mshale.

Wale walioumizwa na tusi lake walijaribu kutoka kumkimbiza lakini hawakumpata.

Jamaa mmoja akasema: “Mashabiki wa Utelembwe ndio walivyo mwacheni msihangaike naye, mtu mwenyewe anaonekana mlevi yule.”

Columnist: www.mwanaspoti.co.tz