Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Bernard Kamungo Shujaa aliyeikomboa familia yake

Kamungo Pic Bernard Kamungo Shujaa aliyeikomboa familia yake

Wed, 2 Aug 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Wiki chache zilizopita winga, Bernard Kamungo alikuwa nchini akitokea Marekani ambako anacheza soka la kulipwa, anakumbuka vile ambavyo yeye na familia yake walivyokuwa hawana mbele wala nyuma eti sasa anatazamwa kama mtu mwenye thamani ambaye anapewa majukumu ya kilipigania taifa hakika Mungu ni wa ajabu.

Kamungo ambaye anaichezea FC Dallas ya Ligi Kuu Marekani 'MLS' alikuwa sehemu ya kikosi cha Adel Amrouche ambacho mwezi uliopita July kilicheza mchezo wa kuwania nafasi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika dhidi ya Niger.

Nyota huyo ambaye alikuwa akiishi katika kibanda cha udongo katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu, Kigoma na wazazi wake na ndugu zake watano, bila umeme miaka mingi iliyopita kabla ya kwenda Marekani, anasema,"Mungu ni mwema pengine hilo ndio neno ambalo linaweza kutosha na kueleza ninayoyawaza na kufikiri."

Heshima ya kuitwa Taifa Stars ni kitu kikubwa kwake na anaamini kuwa anaweza kuwaparaha Watanzania kama ilivyokuwa kwa mashabiki wa FC Dallas ambao walifurahia mno alipofunga bao lake la kwanza kwenye ligi.

Anasimulia kwa kusema, Aprili 15, 2023 alipata nafasi kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Real Salt Lake dakika ya 88 alipachika bao la kusawazisha kwa chama lake.

Wakati umati wa watu ukimzunguka, Kamungo anasema akili yake ilipotea. Alichoweza kufikiria kufanya ni kukimbilia kwenye kona huku timu yake ikimsonga mbele ya umati wa kihistoria wa Uwanja wa Toyota.

"Naona hicho kinaweza kutokea upande wa Taifa Stars sijui ni lini ila wakati wangu unakuja kama ilivyokuwa kwa klabu yangu, nashukuru sana wachezaji wenzangu kwa namna ambavyo wamenipokea vizuri naamini tutaendelea kushirikiana na kunifanya nizoeane nao kwa sababu ile ilikuwa mara yangu ya kwanza kuwa nao pamoja," anasema nyota huyo.

Ilikuwaje Kamungo kutoboa hadi Amerika? Hakukuwa na matumaini makubwa kwa familia yake huko Nyarugusu katika makazi yaliyokuwa na watu 150,000, ambayo yaliundwa mwaka 1996 wakati makumi ya maelfu ya wakimbizi walivuka mpaka kutoroka vita vya wenyewe kwa wenyewe katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Wazazi wa Kamungo walikuwa wameishi kambini kwa miaka sita kabla ya Kamungo kuzaliwa mwaka wa 2002.

Alikulia kambini, akiongea Kiswahili na familia yake na kujifunza Kifaransa katika shule ya wakimbizi huku familia yake ikisubiri kwa hamu idadi yao kuitwa kwa ajili ya makazi mapya. Hata katika umri mdogo, Kamungo alijua hali mbaya ya mazingira yake: aliacha shule kwa siri alipokuwa na umri wa miaka 11.

Hakuwa na moyo wa kuwaambia wazazi wake kwamba alikuwa akienda mahali fulani kando na masomo kila asubuhi.

Watu wanaoishi katika kambi za wakimbizi ni nadra kufikiria kuhusu mipango ya miaka 10. Ni ngumu kujiandaa kwa siku inayofuata, au mlo unaofuata hapa anasimuliwa kwa kusema, "Sikuwa na maono yoyote ya siku zijazo kwa sababu nilikuwa na wasiwasi kuhusu kesho," Kamungo anaendelea, "Nilikuwa nikiishi kwa wakati huo."

Maisha yalibadilika akiwa na umri wa miaka 14, alipojua kwamba Kamati ya Kimataifa ya Uokoaji ingeihamishia familia yake Marekani. Baada ya miongo miwili katika kambi ambapo chakula kilikuwa kigumu kupatikana, ambapo fursa zilikuwa chache, familia ilikuwa na matumaini.

Ingawa alikuwa na maoni yasiyoeleweka ya jinsi maisha ya Amerika yalivyokuwa kutoka kwa sinema na vipindi vya Runinga, hakuwa na matarajio yoyote isipokuwa kwamba kungekuwa na chakula cha kutosha kwa kila mtu. Hilo lingemtosha.

Kamungo amesahau baadhi ya maelezo kuhusu kuwasili kwake Marekani, kuanzia uwanja wa ndege ambao familia hiyo ilitua. (Pengine ilikuwa DFW.) Lakini anakumbuka jinsi ilivyojisikia kufika katika mji wao mpya, Abilene.

Ghafla, akina Kamungo walikuwa na kiyoyozi, mabomba ya ndani vitu ambavyo hawajawahi kuishi navyo hapo awali. Jokofu, pia, ambalo lilikuwa na vyakula visivyojulikana.

Lakini hakuzungumza Kiingereza hata kidogo, na ustadi wake wa lugha ya kawaida na tabia yake ya aibu ilifanya maisha yake ya shule kwa Marekani kuwa magumu.

"Shule ilikuwa nzuri sana," anasema. "Na kuweza kupata chakula katikati ya siku nikiwa shule lilikuwa jambo kubwa kwangu."

Huo ndio ukawa mwanzo wa mafanikio yake, alifanya vizuri hatua kwa hatua na ndipo alipojipata kwa kuamua kujikita kwenye soka ambalo limemtoa na kuwa msaada kwenye familia yake kutoka kula mlo mmoja kwa tabu hadi kuwa na uwezo wa kutengeneza dolla 10,000 kwa wiki, ni zaidi ya Sh24.5milioni.

Columnist: Mwanaspoti