Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Bahili? Toddy aweka kufuru hii ya pesa

Todd Boehly Kigogo wa Chelsea Todd Boehly

Sat, 7 Jan 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kigogo wa Chelsea Todd Boehly yupo mbioni kuweka rekodi ya kutumia Pauni520 milioni ndani ya miezi saba tu tangu ainunue timu hiyo.

Kiasi hicho cha pesa anaweza kukifikia ikiwa mastaa watano wanaohusishwa kuhitajika na timu hiyo watatua katika dirisha hili la majira ya baridi.

Mashabiki wengi wa Chelsea walikuwa wamenyong'onyea wakiamini kwamba zama za kumwaga pesa kwenye madirisha ya usajili zimeisha mara baada ya Roman Abramovich kuiuza timu hiyo kwa Mmarekani Boehly.

Ilikuwa inaaminika kuwa wamarekani wengi hawana mchezo wa kumwaga mwaga pesa kama ilivyo kwa waarabu kwa tafsiri fupi ni mabahili..

Lakini mambo yamekuwa tofauti kwani Boehly hadi sasa ameshatumia Pauni 270 milioni kwenye usajili wa dirisha lililopita ambapo walinunuliwa Wesley Fofana, Marc Cucurella, Raheem Sterling, Kalidou Koulibaly na Pierre-Emerick Aubameyang.

Vilevile walisajiliwa makinda kama Carney Chukwuemeka na Cesare Casadei kwa ajili ya timu za vijana. Kiasi hicho cha pesa kinaweza kuzidi zaidi katika dirisha hili ikiwa mastaa watano wanaohusishwa watatua kwenye kikosi hicho.

Hapa kuna orodha ya mastaa hao na pesa zinazoweza kuwagharimu Chelsea hadi kuwapata na ikiwa itafanikiwa Boehly ataingia kwenye orodha ya matajiri waliotumia pesa nyingi kwenye usajili ndani ya muda mfupi.

ENZO FERNANDEZ - £112m

Unaweza kusema huyu ni namba moja na tayari imeshathibitishwa kuwa Chelsea imeshatuma hadi ofa kwa ajili ya kukamilisha mchakato wa kumchuku.

Enzo ambaye alimaliza michuano ya Kombe la Dunia kwa kuiwezesha Argentina kuchukua ubingwa nayeye kupata tuzo ya mchezaji bora kijana, mabosi wa timu yake Benfica wanataka Chelsea ilipe Pauni 106 milioni yote kwa mara moja ili kumpata wakati Chelse yenyewe ikiomba kulipa Pauni 112 milioni kwa miaka mitatu ili kuepuka rungu la sheria ya matumizi ya pesa kutoka FIFA.

Ikiwa Benfica itaendelea kukaza, Chelsea imepanga kutumia uhusiano mzuri uliopo kati ya kocha wao Gharam Potter na mabosi wa Brighton kuhakikisha inampata kiungo wa timu hiyo

Alexis Mac Allister kama mbadala wa Enzo. Hata hivyo Brighton iliweka wazi kuwa haina mpango wa kumuuza staa huyo katika dirisha hili.

MYKHAILO MUDRYK - £88m

Hapa Chelsea ni kama imeingilia kati na inataka kuitibulia Arsenal, mchongo upo hivi, Arsenal hadi sasa imeshakubaliana na mchezaji lakini changamoto imekuwa kwa Shakhtar Donetsk ambayo inahitaji Pauni 88 milioni.

Kiasi hicho cha pesa Arsenal imekuba kukitoa lakini kwa mafungu, Shakhtar imekataa suala hilo.

Chelsea hapa inadaiwa kuwa tayari kutoa pesa yote kwa pamoja na mazungumzo hadi kufikia sasa yanaendelea na kuna asilimia kadhaa za staa huyo kutua darajani na ikiwa hilo litafanikiwa itazidi kuzidisha ile bili.

BENOIT BADIASHILE - £35m

Monaco inahitaji mpunga usiopungua Pauni 35 milioni ikiwa Chelsea inahitaji kuipata huduma ya fundi huyo.

Kwa sasa Chelsea inahitaji sana kuboresha eneo lao la ulinzi ambalo limekuwa na changamoto kwa msimu huu, huku kuondoka Antonio Rudiger aliyejiunga na Real Madrid ikitajwa kuwa ni sababu moja wapo.

DAVID DATRO FOFANA - £10m Hapa tayari pesa imeshamwagika na wataalamu wa mambo wanamfananisha staa huyu na lejendi Didier Drogba kutokana na uchezaji wake.

Fundi huyu wa kimataifa wa Ivory Coast Fofana ndio mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Chelsea katika dirisha hili na inaelezwa ni mmoja kati ya mastaa ambao Gharam Potter anawakubali sana na alihitaji kumsajili tangu akiwa Brighton.

Columnist: Mwanaspoti