Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Azam ni 4-0 Chamazi

Azam Bao 4 Azam walipoteza kwa magoli 3-0

Wed, 12 Oct 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya Azam kuanza vibaya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuruhusu kuchapwa mabao 3-0 ugenini Libya na Al Akhdar, uongozi, benchi la ufundi na wachezaji wanamatumaini ya kupindua meza kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa Oktoba 16, Azam Complex.

Azam inahitaji ushindi wa mabao 4-0 ili kusonga mbele kwenye michuano na kama mechi itamalizika kwa Azam kushinda 3-0 basi itaamuliwa kwa mikwaju ya Penalti. Kocha mkuu, Mfaransa, Denis Lavagne ameeleza kuwa ; “Kwenye mpira kila kitu kinawezekana, tumepoteza kwa mabao matatu ugenini lakini tunayo nafasi ya kufanya vizuri nyumbani na kushinda zaidi.”

“Ni kiu ya kila mpenzi wa timu hii kuiona ikisonga mbele, hivyo tunarudi kuyafanyia kazi makosa na kuboresha kila eneo ili tuwe imara zaidi katika mechi ya marudiano,” alisema Lavagne.

Nahodha wa Matajiri hao wa Chamazi, Sospeter Bajana alisema; “Kama wachezaji tumeumizwa na matokeo ya mechi ya kwanza, lakini bado tunanafasi ya kufanya vizuri zaidi nyumbani, tunaenda kujipanga.”

Ofisa Mtendaji mkuu wa timu hiyo, Abdulkari Amin ‘Popat’ amefunguka kuwa; “Tupo tayari kuwapokea na kucheza nao, utakuwa ni mchezo mgumu kwetu lakini tumejiandaa kushinda na tunaamini inawezekana.”

Columnist: Mwanaspoti