Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Azam Tv wameanza, CCM nao wamalizie

AZAM FLAG 02 1?fit=825%2C450 Azam Tv wameanza, CCM nao wamalizie

Fri, 19 Feb 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Mwanahiba RichardMore by this Author JUZI Jumanne wadhamini wa Ligi Kuu Bara, Azam Tv walitangaza kuweka taa kwenye viwanja vinne ambavyo vinatumika kwenye mechi za ligi hiyo.

Azam wataweka taa kwenye viwanja vinne ambavyo ni Gwambina uliopo wilaya ya Misungwi unatumiwa na timu ya Gwambina FC, Mkwakwani wa Tanga wenyeji ni Coastal Union, Majaliwa uliopo Lindi unatumiwa na Namungo FC pamoja na Kaitaba mkoani Kagera ambao hutumiwa na Kagera Sugar.

Ni jambo la heri maana huenda wadhamini hao wanaorusha mechi za ligi moja kwa moja (live) wameangalia vitu mbalimbali ambavyo vimesababisha wao kukubaliana kufanya matengenezo hayo ambayo pengine hayakuwahi kufikiriwa na kampuni yoyote ama hata wamiliki wa viwanja hivyo.

Viwanja vingi vinavyotumika na ligi hiyo humilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na vingi vipo katika hali mbaya ambapo hata mwaka jana mzunguko wa kwanza tu viliwahi kufungiwa kwa zaidi ya viwanja vitano ukiachana na Gwambina ambao unamilikiwa na timu pamoja na Kaitaba na Majaliwa.

Viwanja vya Mkwakwani unamilikiwa na CCM na umewahi kufungiwa kutokana na kutokidhi vigezo na vigezo sio kwenye eneo la kuchezea tu (pitch) ambapo ulifanyiwa ukarabati na kuruhusiwa kuendelea kuchezwa mechi za ligi.

Azam wameanza na viwanja hivyo pengine hapo baadaye wataoana ni vyema kuwekwa taa kwenye viwanja vingine, lakini kwanza mpaka pale watakapojiridhisha na miundombinu ya viwanja hivyo kama ilivyo kwenye viwanja hivyo ambavyo wamekaa na kukubaliana kuweka taa.

Columnist: mwanaspoti.co.tz