Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Ally Salim anavyopita njia ya Manula Msimbazi

Ally Salim Gh Ally Salim anavyopita njia ya Manula Msimbazi

Fri, 5 May 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mechi nne za kibabe kwa kipa chipukizi wa Simba, Ally Salim Khatoro zimemtambulisha rasmi kwa wapenzi wa soka nchini kwamba yeye ni kitu kikubwa kijacho (Next Big Thing) kwenye mpira wa Tanzania.

Safari hii ya kusisimua ilianzia kwenye mechi ya watani wa jadi, Aprili 16, ambapo maajabu aliyoyafanya ndiyo sababu ya simulizi hii.

Alipata nafasi kutokakana na kukoseana kwa makipa tegemeo, Aishi Manula aliyekuwa majeruhi, na Beno Kakolanya aliyebainika kusaini Singida Big Stars. Hii ndiyo njia aliyotokea Aishi Manula hadi kufikia hapa alipo leo.

Ilikuwa Machi 19, 2014 kwenye mchezo wa mzunguko wa pili wa ligi kuu kati ya Yanga na Azam FC, uwanja WA Mkapa.

Kipa namba moja wa Azam FC wakati huo alikuwa Wadini Ally, kutoka Zanzibar. Kuelekea mchezo huo, Mwadini akaimba ruhusa aende kuhudhuria msiba nyumbani kwao Zanzibar.

Akaruhusiwa na akaondoka. Lakini viongozi wa Azam FC ni kama machale yaliwacheza.

Wanataka kujiridhisha kama kweli kulikuwa na msiba kwa akina Mwadini. Wakatuma mtu aende kuthibitisha, akafika lakini hakukuta msiba kwao wala kwa jirani...siku hiyo, wiki hiyo wala mwezi huo.

Taarifa zilipowafikia wakuu wa Chamazi, wakasema, 'huyu anataka kutuletea masihara', wakamuondoa kwenye mpango kazi wa mechi.

Kocha Joseph Omog akashirikishwa, akasema hakuna tabu. Kocha wa makipa, Idd Abubakary akasema 'dogo Aishi yuko tayari kwa mchezo'.

Siku ilipofika, Aishi akapewa majukumu. Huu ulikuwa mchezo muhimu sana kwa Azam FC kuelekea mbio za ubingwa. Hadi hapo Azam FC walikuwa wanaongoza ligi kwa alama 4 juu ya Yanga.

Endapo Yanga wangeshinda mchezo huu maana yake wangepunguza pengo la alama hadi moja na kuongeza presha.

Lakini Azam FC hawakuogopa yote hayo, wakamuamini dogo Aishi. Naye hakuwaangusha, aliifanya kazi iliyotukuka kweli kweli.

Aliokoa michomo mingi sana ya Khamis Kiiza na Didier Kavumbagu. Lakini kubwa zaidi aliokoa hadi penati ya Khamis Kiiza.

Mchezo ukaisha kwa sare ya 1-1 na Azam FC wakawa wamelinda uongozi wao wa ligi WA alama 4 juu ya wapinzani wao wa karibu.

Kuanzia hapo Aishi Manula akawa kipa namna moja wa Azam FC hadi alipoondoka mwaka 2017 kujiunga na Simba SC.

Na tangu Aishi aende Simba mwaka huo, amekuwa kipa namna moja licha ya kuletewa changamoto kadhaa ikiwemo ya Beno Kakolanya ambaye wengi wanamheshimu kwa uwezo wake.

Lakini Aprili 16, 2023 jambo geni likatokea. Mtoto kutoka akademi, kama ilivyokuwa kwa Aishi, anapata nafasi kwenye mechi dhidi ya Yanga. Anafanya maajabu na kuzua gumzo kwa waajiri wake hadi mashabiki mitaani.

Aishi alipata nafasi kutokakana na kukosekana kwa kipa aliyetakiwa kudaka siyo. Alikosekana kwa sababu watu hawakuwa na imani naye kufuatia taarifa za kiintelijensia.

Ally Salim naye amepata nafasi kutokana na kukosekana kwa kipa aliyetakiwa kudaka siku hiyo. Alikosekana kwa sababu watu hawakuwa na imani naye kufuatia taarifa za kiintelijensia.

Je Ally Salim atafanya kama Aishi, kuishikilia namba jumla jumla na kuwa namba moja wa klabu yake na nchi kwa ujumla?

Columnist: Mwanaspoti