Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

ATM YA WIKI: Kazi bure Maguire anavyotia hasara Old Trafford

Maguire Harry Mm Mlinzi wa Man United, Harry Maguire

Tue, 22 Mar 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Mambo yamebadilika sana kwa eki kisiki wa Manchester United na England ambaye tangu atue Jijini Manchester kujiunga na wababe hao akitokea Leicester City amekuwa na kiwango kibovu sana ambacho hakionekani kuwaridhisha mashabiki wa timu hiyo.

Lakini jambo la kushangaza ni kwamba licha ya kiwango kibovu anachoonyesha bado akaunti zake za benki zimeendelea kuwa kwenye hali nzuri na anaishi maisha ya kibosi sana. Kiujumla anakadiriwa kuwa na utajiri unaofikia Pauni 25 milioni ambayo ni zaidi ya bilioni 50 za Kitanzania.

ANAPIGAJE PESA?

Anapata pesa kupitia mshahara wake wa kila wiki ambao ni Pauni 195,000 ambayo kwa mwaka huwa ni Pauni 10 milioni kutokana na mjumuisho wa bonasi.

Mbali ya mshahara huo wa kibosi anapata pesa pia kupitia madili kibao ya nje ya uwanja. Miongoni mwa kampuni ambazo anafanya nazo kazi kama balozi wao ni Puma aliyosaini nayo mkataba wa ubalozi mara baada ya kujiunga na Man United, mkataba huo una thamani ya Pauni 700,000 na kila mechi anayocheza huku mguuni akiwa na viatu kutoka kampuni hiyo, huwa anakunja Pauni 18,000 ambayo ni zaidi ya milioni 40 za Kitanzania.

Mbali ya kuvaa viatu, jamaa amekuwa akiitangaza kampuni hiyo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii kwa kutupia picha mbali mbali akiwa amevalia mavazi yenye nembo yao.

NDIGA

Januari mwaka 2013, alinunua gari aina ya Audi A5 S Line ambayo amedumu nayo hadi sasa lakini mbali ya hilo anamiliki gari nyingine kadAhaa aina ya Range Rover ambazo mbili na ndio amekuwa akionekana kuzitumia zaidi wakati anawasili kwenye mazoezi ya timu au akiwa kwenye misele ya kawaida. Jumla ya gari zake zote zinakadiriwa kuw ana thamani ya Pauni 5 milioni.

NYUMBA

Anaishi Jijini Manchester, lakini nyumba yake haijajulikana hasa ipo maeneo gani kwani jamaa amekuwa hana desturi ya kuweka hadharani maisha yake binafsi.

MSAADA KWA JAMII

Amekuwa akijitoa zaidi kwenye kusaidia jamii, Mei mwaka huu alipewa tuzo PFA’s Community Champion kutokana na mchango wake mkubwa wa kusaidia taasisi ya Manchester United Foundation.

Pia aliwahi kuwa sehemu ya mastaa walioungana na jamii kwenye kuchangia vyakula kwenye taasisi mbali mbali za watoto wa yatima wakati England imezuia shughuli mbali mbali za kijamii kutokana na kushamiri kwa janga la Uviko 19.

MAISHA BINAFSI

Yupo kwenye uhusiano na mrembo Fern Hawkins ambaye amekuwa naye kwenye uhusiano kwa kipindi cha miaka 10 na mwaka April, 3, 2019 walifanikiwa kupata mtoto wao wa kwanza waliyempa jina la Lillie Saint Maguire. Vilevile walijipatia mtoto wa pili Mei, 2020, aitwaye Piper Rose.

Kwenye suala la bata jamaa pia yumo. Mara kadhaa amewahi kuonekana akiwa kwenye kumbi kumbi mbali mbali usiku akiwa na washkaji zake wakinywa pombe.

KWENYE MITANDO YA KIJAMII

Ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter ana wafuasi milioni moja, Instagram milioni mbili na Facebook ni milioni mbili pia na kote huko anapiga pesa.

Columnist: www.mwanaspoti.co.tz