Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

2022 ulikuwa mwaka wa Dabi

Simba Vs Yanga 2022 ulikuwa mwaka wa Dabi

Mon, 19 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Siku zinahesabika kabla ya Mwaka 2022, kusepa kuupisha 2023, huku kukiwa na kumbukumbu nyingi za kusisimua.

Katika soka achana na mafanikio kwa timu kadhaa zikiwemo za walemavu, Serengeti Girls, huku Simba na Yanga zimefanya kweli anga za kimataifa, lakini 2022 ulikuwa mwaka wa Dabi.

Timu hizo zimekutana mara nne katika mechi za mashindano tofauti, huku Yanga ikitamba kwa kutopoteza mbele ya watani wao.

Yanga imeshinda mechi mbili, huku mbili zikiisha kwa sare, pia ikifunga mabao manne na kufungwa mawili.

Makala hii inakuletea michezo minne miamba hiyo ikijumuisha miwili ya Ligi Kuu Bara na mingine ya Ngao ya Jamii na Kombe la ASFC.

KAZI ILIANZA HIVI

Simba na Yanga ziliuanza mwaka 2022 katika mechi ya marudiano ya Ligi Kuu msimu uliopita iliyopigwa Aprili 30 na kumalizika kwa suluhu.

Kabla ya mechi hii, Simba ilipewa nafasi kubwa ya kupata ushindi kutokana ilivyoonekana kuimarika na pia kutaka kulipa kisasi, lakini ikakwama.

KIPIGO KIRUMBA

Mei 28, wababe hao walikutana tena CCM Kirumba, jijini Mwanza kwenye emchi ya nusu fainali ya ASFC na Yanga kushinda 1-0 na kwenda fainali.

Yanga iliingia fului mkoko, tofauti na watani wao waliokuwa na kikosi dhaifu kwani iliwakosa nyota wa kikosi cha kwanza kama, Shomary Kapombe, Aishi Manula, Clatous Chama na wengine.

Bao la dakika 25 la Feisal Salum ‘Fei Toto’, lilitosha kuivua taji Simba, huku Yanga ikienda fainali na kubeba ndoo kwa kuifumua Coastal Unioni mechi iliyopigwa Arusha.

NGAO TENA

Agosti 13, vigogo hao walifungua msimu wa 2022-2023 kwa kukutana katika mechi ya Ngao ya Jamii ikiwa ni mara ya pili mfululizo, kwani msimu uliopita zilikutana na Simba kuchapwa bao 1-0.

Katika mechi hiyo, Yanga ilitamba tena kwa kuifunga Simba mbao 2-1, licha ya kutanguliwa kwa bao la mapema la kipindi cha kwanza la Ousmane Sakho.

Fiston Mayele alifunga mara mbili na kuendeleza ubabe wake kwa Simba katika Ngao ya Jamii, kwani msimu uliopita pia alifunga.

SARE YA OKTOBA 23

Mechi ya mwisho kwa watani ndani ya 2022 ilipigwa Oktoba 23 na kumalizika kwa sare ya 1-1.

Simba ilikuwa na matumaini makubwa ya kufuta unyonge kwa Yanga kwa bao la utangulizi la Augustine Okrah, lakini mkwaju wa frikiki ya dakika za majeruhi kabla ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza kiliitibulia.

Aliyewanyima raha alikuwa ni Stephane Aziz KI aliyepiga kiufundi mkwaju wake na kumuacha Aishi Manula akigaragara chini.

Hiyo ilikuwa ni sare ya tatu mfululizo kwa watani katika Ligi, tangu Yanga ilipoinyoa Simba kwa bao 1-0 mechi ya kufungia msimu wa 2020-2021, likiwekwa wavuni na kiungo Zawadi Mauya.

Mara ya mwisho Simba kuitambia Yanga katika ligi ilikuwa mwaka 2019 wakati Meddie Kagere alipokwamisha kimiani mpira wa kichwa. Mwaka 2023 utakuwaje? Tusubiri!

Columnist: Mwanaspoti