Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

jinix66: Mashabiki hawanijui, wanafahamu kazi zangu

Jini XX Mwanamuziki na producer Geniusjinix66

Wed, 20 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki na producer Geniusjinix66 amedai kuwa mashabiki wake asilimia 99 hawamfahamu lakini wanapenda kazi zake.

Genius akiwa kwenye mahojiano na BBC Swahili ameeleza kuwa anaona bora kazi zake ziongee kwa mashabiki kuliko yeye, huku akitolea mfano wimbo wake wa 'Juu' ambao umefanya vizuri katika mitandao ya kijamii, huku wengi wakidhani kuwa wimbo huo ni wa Jay Melody.

Hata hivyo amezungumzia kuhusiana na msaada wa mtandao wa TikTok kwa wasanii wachanga kwani ngoma zao zimekuwa zikifanya vizuri na kutumiwa na watu wengi kwenye mtandao huo ikiwemo yeye mwenyewe nyimbo zake zi mekuwa zikipendwa na kupata watu wengi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live