Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zuwena: Mwanangu amekuwa staa shuleni

Zuwena Hdr Mwanangu amekuwa staa shuleni

Wed, 19 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Video Vixen wa wimbo wa Diamond Platnumz 'Zuwena' anayejulikana kwa jina la Zuwena mitandaoni huku jina lake la halisi likiwa ni Recho amezungumza sababu za kuchora Tattoo ya Diamond mwilini mwaka.

Recho/Zuwena amesema kuwa hiyo yote ni kama shukrani kwa Diamond maana amemtoa sehemu ambayo alikuwa hajulikana na sasa anajulikana nchi nzima na nje ya nchi.

Recho ameongeza kuwa yeye ni msanii wa uigizaji na ameifanya kazi hiyo miaka 10 lakini alikuwa hajulikani ila Diamond amemfanya ajulikane hivyo ametoa shukrani kwake.

Recho ameeleza kuwa anamiliki nyumba na ana mtoto wa miaka 15 ambaye anampenda sana Diamond.

"Sasa hivi mwanangu ni staa shuleni kwao, huko shuleni wananijua, wanafunzi wenzake na huwa wanamtania mwanagu.

"Nilipofanya nyimbo na Diamond mwanangu alinipigia simu kutoka shuleni kwao Kibaha akaniambia kwa hiyo mama umekuwa staa?

"Ikifika muda wa kulipa ada kama sijalipa mwanangu anataniwa sana na walimu wakinipia simu wananiambia wewe msanii mwanao anadaiwa ada huku,” amesema Zuwena.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live