Mhubiri maarufu jijini Mwanza asiyeishiwa vituko, Diana Bundala maarufu kama "Mfalme Zumaridi" amemvaa tena mama wa aliyekuwa msanii wa Bongo Movies, Steven Charles Kanumba, mama Flora Mtegoa 'Mama Kanumba'.
Mfalme Zumaridi amefunguka kuwa aliwahi kumtumia tiketi ya ndege Mama huyo kwenda Mwanza kwa ajili ya kumhsuhudia mwanaye huyo ambaye alishafariki dunia tangu Aprili 7, 2012.
Povu la Zumaridi linakuja baada ya Mama Kanumba kumtaka mchungaji huyo amuache kwani amekuwa akitonesha kidonda chache cha maumivu ya kifo cha mwanaye kipenzi kwa kudai kuwa bado yupo hai na atamfufua hivi karibuni.
"Mama Kanumba tulimkatia tiketi ya ndege akaja mpaka hapa, alilala nyumba hiyo (anaionyesha) tena chumba kizuri na tukampikia akala vizuri.
"Baada ya hapo nikamwambia anayemuona Kanumba ni binti huyu, ndiyo anayemhudumia kila kitu na kuongea naye, wakaanza kuongea na mwanaye.
"Mambo waliokuwa wanayaongea ni ya ndani yule mama anayajua mpaka akaanza kulia. Akasema ana presha na mambo yanayoongelewa ni kama yupo na Kanumba. Akaomba apumzike.
"Nikamwambia aongee kwenye media yale aliyoyashuhudia na kuzungumza na mwanaye kuwa yupo na ipo siku atakuja. Mama yule alikataa akasema anaogopoa hawezi kusema kwenye media pia bado ana kesi na Lulu.
"Lakini baada ya hapo mama Kanumba akataka hela, akasema ili aongee aliyoyaona nimpe Tsh milioni 1, kwa sababu mwanaye ni maarufu hivyuo akiongea atanipa mimi umaarufu, mimi sikumpanga na sijawahi kumpanga mtu.
"Nikasema siwezi kukupa hela kwa sababu yaliyotokea ni ya kweli, nikikupa hela kama nakupa rushwa. Mimi sio wa kukosa milioni moja kumpa Mama Kanumba. Kama ningekuwa natafuta kiki ningempa palepale ili atangaze uongo.
"Yeye aendelee kutukana na kudhihaki, ila ajue Kanumba yupo hai na ipo siku atamuona, sio yeye tu, hata watu wengine mtawaona kwa macho ya damu na nyama na kushuhudia ninachokisema, na si muda mrefu.
"Kanumba ameletwa na Mungu, kwa sasa sio zombi, Mungu ametumia gharama kubwa kumleta Steve katika hali yake ya kawaida. Naweza nikamleta mtu yeyote hapa akaongea na Kanumba moja kwa moja, sina uongo," amesema Zumaridi.