Mmiliki mwenza wa mtandao wa Meta na Facebook, Mark Zuckerberg amepanda cheo na kuwa mpambanaji wa mkanda wa bluu katika mtindo wa mapigano wa Kibrazil wa Jiu Jitsu.
Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Zuckerberg ameandika: "Nimepewa heshima ya kushindana katika mkanda wa bluu na timu ya Guerrilla San Jose.” kabla ya Mwigizaji na bingwa mwenzake wa Jiu Jitsu wa Brazil, Tom Hardy kuacha maoni akimpongeza Zuckerberg kwa mafanikio hayo.
Hata hivyo, si mara ya kwanza kwa uwezo wa Zuckerberg kushika vichwa vya habari, kwani mapema mwaka huu bilionea huyo wa teknolojia alishiriki mashindano ya Jiu Jitsu huko California ambapo baadaye alifichua katika mahojiano na Lex Fridman kwamba alihudhuria mashindano hayo kwa siri ili mtu yeyote asimtambue.
Kuna rangi tano tofauti za mikanda katika mtindo wa upiganaji wa Jiu Jitsu wa Brazili, inayoanza na mkanda mweupe, mkanda wa bluu (Blue belt), mkanda wa zambarau, mkanda wa kahawia na kisha mkanda mweusi (Black belt) ambao huweza kumchukua mtu zaidi ya miaka 10 kuupata mkanda mweusi kwenye Jiu Jitsu ya Brazili.
Haya yanajiri takribani mwezi mmoja baada ya Zuckerberg na bilionea mwenzake wa teknolojia na Musk kukubaliana kupigana katika pambano la mtindo wa UFC.
Musk ndiye alikuwa wa kwanza kumchokoza Zuckerberg kwa kumtaka wapande ulingoni kupigana baada ya Zuckerberg kumuita mchumba katika moja ya tweet zake. Baadae Zuckerberg alimjibu kwa kumtaka Musk amtumie jina la eneo la mapigano hayo.
Mvutano kati ya wawili hao umeonekana kuwa mbaya zaidi hadi kupelekea Zuckerberg kuzindua mtandao wa Threads, ambao umeleta upinzani mkubwa kwa mtandao wa Musk wa Twitter.
Ingawa hakuna tarehe rasmi iliyowekwa kwa ajili ya pambano lao hilo lakini hatua ya Zuckerberg kutawadhwa kama mpambanaji wa mkataba wa blue ni litamfanya Musk ajihadhari sana akitambua mpinzani wake ni mtu wa viwango gani.