Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zuchu namba moja Afrika, awakalisha kina Yemi Alade

Zuchu Kudhalilishwa Zuchu namba moja Afrika, awakalisha kina Yemi Alade

Tue, 25 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva kutoka katika lebo ya WCB Wasafi chini ya Nasibu Abdul alimaarufu Diamond Platnumz, Zuhuru Othmani 'Zuchu' amekuwa msanii namba moja katika bara la Afrika kwa wasanii wa kusini mwa Jangwa la Sahara kwa kuwa na wafuasi (Subscribers) wengi katika mtandao wa Youtube.

Kabla ya Zuchu kushika namba moja Youtube kwa wasanii wa kike, nafasi hiyo alikuwa anaishikilia msanii kutoka Nigeria Yemi Eberechi Alade.

Kasi ya Zuchu ni kubwa sana na ikumbukwe ni msanii ambaye hajamaliza hata miaka minne baada ya kutambulishwa rasmi WCB na kufungua mitandao yake mfano Youtube ukilinganisha na wasanii wakongwe kama Yemi Alade, Tiwa Savage na wengine.

Zuchu aliifungua akaunti yake ya Youtube rasmi Jan 29, 2019 huku Yemi Alade akifungua Nov 15, 2012.

Hii hapa ndio Orodha ya wasanii wanaoongoza kwa Subscribers katika mtandao wa Youtube.

1. Zuchu -2.29M 2. Yemi Alade -2.10M 3. Sinach -1.97M 4. Ada Ehi -1.147M 5. Tiwa Savage -1.14M 6. Nandy -1.11M 7. Symplysimi -0.87M 8. Diana Marua 0.78M

Chanzo: www.tanzaniaweb.live