Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zuchu kukiwasha Simba Day

Simbasctanzania 296321184 1632518510481861 1443203850317451135 N Zuchu na Barbara

Mon, 1 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Fleva kutoka Lebo ya WCB Wasafi, Zuchu anatarajiwa kutumbuiza katika tamasha la Siku ya Simba 'Simba Day' ambalo litafanyika Jumatatu ijayo, Agosti 8, 2022.

Simba SC wamethibitisha hilo kupitia kwa Ofisa Mtendaji wake, Barbara Gonzalez wakati wa uzinduzi wa wiki ya Simba jana Jumapili, katika Viwanja vya Mbagala Zakhiem, hii itakuwa ni mara ya pili kwa Zuchu kutumbuiza katika tamasha hilo kubwa.

Kwa upande wake Zuchu amesema; "Kuanzia leo, mpaka kufikia kilele cha Simba Day 2022 ni hatulali na watatuchoka, naomba niwafundishe kibwagizo kimoja tu, kuwatumia ujumbe ndugu zetu.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live