Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zuchu kuchuana na Burna Boy MTV EMA Awards 2022

ZUCHU TUZO Zuchu kuchuana na Burna Boy MTV EMA Awards 2022

Wed, 12 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mrembo kutoka WCB, Zuhura Othman ameteuliwa kuwania tuzo kubwa duniani za MTV EMA ambapo ametajwa katika kipengele cha Best African Act (Msanii Bora wa Afrika-2022).

Kwenye tuzo hizo, Zuchu atachuana na mastaa wakubwa wa Afrika Burna Boy (Nigeria), Ayra Starr (Nigeria), Musa Keys (Afrika Kusini) na Black Sherif wa Ghana.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Zuchu amewashukuru mashabiki wake kwa kuchangia mafanikio hayo makubwa.

“Tanzania stand up your girl is nominated on the MTVEMA, god is good niseme asante ni kwa sababu yenu ndo mimi niko hapo nawapenda sana im coming back with a better caption cos right now am still shaking let me calm down first,” aliandika Zuchu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live