Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zuchu kanizidi kila kitu hadi sura - Gigy Money

Gigy Na Zuchu Zuchu kanizidi kila kitu hadi sura - Gigy Money

Mon, 18 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii na mwokovu Gigy Money ameingia live kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo alikuwa akijibu baadhi ya maswali ya mashabiki zake, moja ya swali aliloulizwa ni kwamba kwanini unamuonea wivu Zuchu? au kwasababu kakuzidi kila kitu? na haya ndiyo majibu yake.

Gigy alisema hawezi kumuonea wivu Zuchu ila anamuacha ajinyumbue anavyotaka kwasababu kwake kuwa kwenye mahusiano na Diamond Platnumz anaona ni kitu kikubwa sana wakati yeye alishapita hizo levo

"Yes of course Zuchu ananizidi kila kitu kuanzia pesa na hata kukomaa sura vyote kanizidi, lakini asijione sipesho sana kuwa na Diamond wengine hizo levo tulishapita na tunamuangalia Diamond kama msanii na siyo Diamond kama mpenzi wa Zuchu," amesema Gigy.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live