Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zuchu atangazwa balozi wa Zantel 4G

Zuchu Zuchu atangazwa balozi wa Zantel 4G

Mon, 24 May 2021 Chanzo: ippmedia.com

Tukio la utiaji saini makubaliano hayo lilifanyika jana katika makao makuu ya Zantel yaliyopo eneo Amani - Zanzibar na kushuhudiwa na menejimenti ya Wasafi pamoja na waandishi wa habari.

Mkuu wa Biashara wa Zantel, Aneth Muga, alisema kampuni hiyo ina imani kubwa na msanii huyo kutokana na ukweli kuwa ni moja ya kipaji kutoka Zanzibar na anaufahamu vema mtandao wa Zantel.

“Zantel kwa sasa tunaendesha kampeni yetu inayojulikana kama ‘Pasua Anga Ki Zantel 4G’ ambayo inalenga kufanya uelimishaji juu ya matumizi yenye tija ya mtandao wa 4G. Zuchu amekuwa mfano mzuri wa namna anavyotumia mtandao wa 4G kuendeleza kipaji chake na ameweza 'Kupasua Anga Kitaifa na Kimataifa,” alisema Muga.

Aliongeza kuwa, mbali na uelimishaji, kampeni hiyo imelenga kuinua na kutambua vipaji kwenye nyanja mbalimbali ikiwamo za michezo, muziki pamoja na uchekeshaji ‘comedy’.

“Sote ni mashahidi juu ya namna gani msanii huyu alivyoweza ‘Kupasua Anga’ na kuwa mmoja wa wasanii wa kike mashuhuri hapa nchini. Zuchu anakwenda kuwa balozi wa kampeni yetu hii ya 'Pasua Anga Ki-Zantel 4G' ambayo itafanyika kwa muda wa miezi sita mfululizo,” alisema.

Akizungumza baada ya kusaini makubaliano hayo, Zuchu alisema: “Nimefurahi sana kuwa balozi wa kampeni hii ya Pasua Anga Ki Zantel 4G, ukizingatia mimi ni moja ya wasanii kutokea Zanzibar, hivyo naifahamu vizuri Zantel,” alisema na kuongeza

“Intaneti ni kitu muhimu sana kwangu, siwezi kukaa saa 24 bila kuwa na mtandao hasa mtandao wa 4G ambao utaniwezesha kufanya mambo mbalimbali kwa haraka zaidi,” alisema Zuchu.

Chanzo: ippmedia.com