Kampuni ya habari kutoka Africa Magharibi, Avance Media imetoa orodha ya vijana 100 katika bara la Afrika ambao walikuwa na ushawishi mkubwa mwaka 2022.
Katika orodha hiyo, taifa la Nigeria limeongoza kwa kuwa na vijana 31, Kenya imewakilishwa na vijana 11 huku Tanzania wakiwa na vijana saba.
Miongoni mwa Watanzania waliopata nafasi ni Kili Paul, Zuchu, Mbosso, Jokate Mwegelo, Barbara Gonzalez na Millard Ayo.
Hata hivyo, kumekuwa na mjadala kwa vijana haswa kutoka ukanda wa Afrika Mashariki ambao hawakuonekana kwenye orodha hiyo licha ya wengi kudhani wana ushawishi mkubwa.
Kwa mfano Diamond Platnumz, Harmonize, Rayvanny na Alikiba hakuna hata mmoja aliyejinafasi kwenye orodha hiyo.