Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zuchu ashindwa kufikia rekodi yake ya mwaka 2021

Zuchu Kudhalilishwa Zuchu

Mon, 9 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa Bongofleva kutokea WCB Wasafi, Zuchu ameshindwa kuifikia rekodi yake aliyoiweka mwaka jana kusini mwa Jangwa la Sahara licha ya kutoa kazi nyingi ikilinganisha na mwaka uliopita.

Zuchu alisainiwa WCB Wasafi, lebo yake Diamond Platnumz Aprili 2020 akiwa ni msanii wa pili wa kike baada ya Queen Darleen na kutoa EP yake ‘I Am Zuchu’ yenye nyimbo saba zilizomtambulisha.

Mwishoni mwa mwaka jana video ya wimbo wake ‘Sukari’ iliandika rekodi kama video ya muziki iliyotazamwa zaidi YouTube kusini mwa Jangwa la Sahara ikiwa na ‘views’ zaidi ya milioni 60, huku ukifuatiwa na ‘Essence’ ya Wizkid iliyokuwa na ‘views’ milioni 53.

Wimbo huo wenye mahadhi ya Afro Pop ulitoka rasmi Februari 19, 2021 ukiwa umetayarishwa na Maprodyuza wawili; Trone na Lizer Classic ambaye ni Prodyuza rasmi wa WCB Wasafi.

Hata hivyo, mwaka 2022 mambo yamebadilika kwa Zuchu kwani rekodi yake imevunjwa na Staa wa Nigeria, Rema kupitia video ya ngoma yake ‘Calm Down’ yenye ‘views’ zaidi ya milioni 300, huku remix ya ngoma hiyo akimshirkisha Selena Gomez ikichukua nafasi ya pili ikiwa na ‘views’ zaidi ya milioni 190.

Kwa mwaka huu video ya Zuchu iliyotazamwa zaidi YouTube ni ya wimbo ‘Kwikwi’ yenye ‘views’ milioni 17, kisha ikifuatia na video ya wimbo ‘Mwambieni’ yenye views zaidi ya milini 14.

Baada ya video ya wimbo wa Rema ‘Calm Down’ kuongoza kusini mwa Jangwa la Sahara, inafuatiwa na video za nyimbo kama; Last Last – mil. 140 (Burna Boy), Buga – mil. 108 (Kizz Daniel), For My Hand – mil. 70 (Burna Boy).

Nyingine ni Finesse – mil. 61 (Pheelz), Emiliana – mil. 57 (Ckay), Ku Lo Sa – mil. 54 (Oxlade), No Wahala Remix – mil. 53 (1da Banton) na Rush – mil. 52 (Ayra Starr).

Kwa matokeo hayo, Zuchu ameshindwa hata kuingia 10 ya wasanii wenye video zilizotazamzwa zaidi YouTube kwa mwaka 2022 kusini mwa Jangwa la Sahara licha ya kuongoza mwaka uliopita.

Wimbo wa Diamond Platnumz ‘Mtasubiri’ akimshirikisha Zuchu, video yake ndio inaongoza kutazamwa YouTube Tanzania kwa mwaka huu ikiwa na ‘views’ milioni 24, hivyo hata kupitia kolabo hiyo Zuchu ameshindwa kuifikia rekodi yake.

Ikumbukwe kwa mwaka 2020 video ya wimbo wa Diamond Platnumz ‘Jeje’ ndio iliongoza ikimaliza mwaka na ‘views’ zaidi ya milioni 40, huku msanii wa Nigeria, Simi ndiye alishikilia nafasi ya pili kupitia video ya wimbo wake ‘Duduke’ iliyopata ‘views’ zaidi ya milioni 29.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live