Msanii wa Bongo Fleva kutoka Lebo ya WCB, Zuchu amesema kuwa amepata ajali ya gari iliyoumiza goti lake.
Kupitia ukutrasa wake wa Twitter, Zuchu amethibitisha kupata ajali hiyo ikiwa ni siku moja kabla ya kusafiriu kwenda nchini Nigeria kwa ajili ya shoo yake ya hivi karibuni.
Hata hivyo, Zuchu hajaeleza kuwa ajali hiyo imetokea wapi, lini, kwa namna gani na iwapo alikuwa na watu wengine kwenye gari, na hali yake ainaendeleaje mapaka sasa.
"Nimepata ajali ndogo iliyo umiza goti langu jana, siku moja kabla ya safari yangu kwenda kuperform kwenye show ya Muhimu kwangu nchini Nigeria. Canceling a show is one of the hardest decisions siwezi as an artist leo ndo nimejua. Nitakwenda hivyohivyo," amesema Zuchu.