Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zuchu amvaa Ostaz Juma, kumburuza mahakamani

Ostaz Na Zuchu Zuchu amvaa Ostaz Juma, kumburuza mahakamani

Mon, 12 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mrembo kutoka Wasafi Classic Baby (WCB), Zuhura Othman 'Zuchu' amemvaa vilivyo mdau wa burudani Ostaz Juma Namusoma kwa kitendo alichokiita kuwa ni udhalilishaji.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Zuchu ameposti kipande cha video kinachomuonesha Ostaz akizungumza maneno ya kumdhihaki maumbile yake ambapo Zuchu amesindikiza video hiyo na ujumbe uliosomeka hivi:

"Sijawahi kutafuta heshima kwa wanaadamu sipotezi muda na si hulka yangu .Lakini nadhani kuna Muda Inabidi Ufundishe watu namna Ya kukuheshimu. Mimi ni Binti mwenye ndugu, Marafiki na Familia inayonizunguka lakini pengine pia Ni kioo kwa watu kadhaa .Halikadhalika mamayangu Mzazi LEGENDARY Nguli alieipa Tasnia hii Heshima kashiriki kampeni toka za Mwalimu nyerere Mpaka Raisi wetu wa sasa mpendwa Mama yetu Mama samia.

Hajawahi mdhihaki mtu si mgomvi na najua wazi kwa ufahamu wangu hatumjui Kabisa huyu baba. Nadhani Imefika wakati sasa Tuwe na hakiba ya Maneno huu umaarufu wa kuutafuta Bila Vipaji Matokeo yake huwa si Chanya. Nipo kwenye mazungumzo na Taasisi Zinazojihusisha Na haki za Wanawake Bado natafuta muongozo sahihi Kama mpo naomba ushiriakiano wenu.

Mimi si mkamilifu kweli Lakini kuongelea maumbile yangu na ya mzazi wangu Na kutudhalilisha kwa lengo la kujipatia faida ya kimitamdao Sidhani kama ni sahihi @tcra_tanzania NAOMBA MUONGOZO. Nimeongea na Manager wangu tayari tunalishughulikia hili kisheria sijapenda na sifurahishwi na dhihaka za makusudi kama hizi. BABA ULIETENGENEZA MAUDHUI HAYA UJUMBE WANGU WA WAZI UKUFIKIE NASEMA ASANTE NA TUKUTANE KWENYE MKONO WA HAKI."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live