Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zuchu amuonea wivu paka wake kupata mimba

Zuchuu Zuchu amuonea wivu paka wake kupata mimba

Wed, 5 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zuchu; ni malkia mwingine wa muziki wa Kizazi Kipya nchini Tanzania, ambaye analia na kusikitishwa na kitendo cha paka wake kupachikwa mimba ilihali yeye hana.

Zuchu ambaye kumekuwa na tetesi kuwa anatoka kimapenzi na bosi wake Diamond Platnumz anasema kuwa, kitendo hicho kimemdhalilisha kwa kuwa ataonekana hajui kulea.

“Yaani paka wangu wameshampa mimba sasa hivi, mimi mama yake sina mimba, lakini yeye amepata mimba, kwa nini? Amenidhalilisha sana, ninaonekana mama gani mimi ambaye sijui kulea,” anasema Zuchu.

Baadhi ya wafuasi wake, naye wamemuomba ambebee mimba Diamond maana akichelewa sana atakuta mwana si wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live