Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zuchu akiniangamiza nitakwenda peponi - Mwijaku

Mwijaku Zuchu(1) Zuchu akiniangamiza nitakwenda peponi - Mwijaku

Wed, 13 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya mdau wa masuala ya burudani nchini, Burton Mwemba 'Mwijaku' kuchafuana vikali katika mtandao wa Instagram na Khadija Kop ambaye ni mama yake na msanii Zuchu, wawili hao waliombana radhi na kuweka sawa mambo yao.

Sasa msanii huyo wa WCB Wasafi amedaiwa kuibuka na kuapa kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mtangazaji Mwijaku kisa kumdhalilisha mamake bayana machoni pa watu mitandaoni.

Wawili hao walijibizana na kuchafuana kwa maneno kiasi kwamabu suala hilo limemuuma sana Zuchu na kukiri kwamba hawezi kukaa pembeni akiona mamake akidhalilishwa kisa yeye.

Mwijaku amedai kuwa, Zuchu ameapa kutumia pesa zake kumpoteza kabisa jambo ambalo yeye anasema hata akama akifa atakwenda peponi. Msikie Mwijaku;

"Nimemalizana na Khadija Kopa baada ya kumuomba msamaha amenisamehe na amenishauri nitumie njia nzuri ya kuwakosoa watu.

"Lakini nimesikia Zuchu anasema atatumia pesa zake zote benki kuniangamiza, nimwambie tu Zuchu kama hizo pesa anazo kweli azitumie tu kwasababu mimi nakataza zinaa ili kuitafuta pepo.

"Kwangu mimi maisha ya dunia si kitu kwangu, napenda aniangamize kwasababu nakufa nikiwa namtetea Mwenyezi Mungu na Sunna ya Mtume Muhammad raha ilioje.

"Nakuja kufufuliwa naambiwa Mwijaku aliangamizwa na Zuchu baada ya kusimamia maelezo ya Mtume Muhammad. Mkumbusheni atumie pesa zake aniangamize.

"Zuchu na Diamond wote ni wapotevu huwezi kujisifia hadharani eti umezini na watu kadhaa, dunia na vilivyomo visitusahaulishe misingi ya dini yetu ya Kiislamu," amesema Mwijaku.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live