Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zuchu ajisalimisha BASATA kuomba radhi

Zuchu Mwesh Zuchu ajisalimisha BASATA kuomba radhi

Tue, 5 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii Zuchu kutoka Lebo ya Muziki WCB Wasafi siku amefika ofisi za Baraza la Sanaa hapa nchini BASATA kuomba msamaha kwa kuimba tusi katika show yake ya Full Moon Party iliyofanyika visiwani Zanzibar Februari 24, 2024.

BASATA wamethibitisha hilo kupitia mtandao wa Instagram kwa kuweka wazi barua ya Zuchu inayoomba radhi kwa kosa hilo, barua hiyo inasomeka hivi;

"KUOMBA RADHI kwa wapenzi wetu wa sanaa, napenda kutumia fursa hii kuwaomba radhi kutokana na maneno niliyoyatumia kwenye kibwagizo ambacho kilileta taharuki kwenye tamasha la Full Moon Party - Kendwa Beach Zanzibar hivi karibuni’.

"Najua kuwa maneno yameleta sintofahamu kwa wengi wenu na kuleta maana hasi kwa jamii na mashabiki zangu kiujumla’.

"Nia yangu ilikuwa kuleta burudani njema na furaha kwa mashabiki wangu wote, si lengo langu kupotosha, kumomonyoa maadili au kuleta taharuki kwa yeyote’. Ninaomba radhi tena kwa jamii na Baraza la Sanaa (BASATA) ambao ndio walezi wangu," imesema barua ya Zuchu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live