Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zuchu ajibu kauli ya Diamond kuhusu kujiondoa WCB na kulipa bilioni 10

Diamond Zuchu K Zuchu na Diamond

Fri, 19 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii maarufu kutoka Tanzania Zuchu, kupitia kwenye mahojiano na Wasafi TV amesema kwamba hana shida kulipa bilioni iwapo atataka kujiondoa katika lebo ya WCB inayomilikiwa na staa wa Bongo, Diamond Platnumz.

Hii ni baada ya Diamond kumjibu shabiki aliyemuuliza kuwa Zuchu atalipa kiasi gani cha pesa akitaka kujiondoa katika lebo hiyo ambapo alisema kwamba Zuchu atatakiwa kulipa Tsh bilioni 10 iwapo msanii huyo angetaka kutoka kwenye lebo hiyo. "Aahh huyo si chini ya 10 billion si unaona manamba yake huko mjini YouTube baba,"alijibu Diamond.

Akijibu kauli ya bosi wake, Zuchu alisema; "Msanii anapoamua kubaki au kuondoka kwenye lebo naamini kila mkataba una makubaliano yanayopendelea pande zote mbili, ulikaa na kukubaliana, ikiwa ni shimo uliloingia ulichimba hela mwenyewe.

"Ikiwa kuna mambo ulitaka yabadilishwe ulikuwa na nafasi ya kufanya hivyo mwenyewe. Kila kitu kinajadiliwa, wasanii walikuwa wanaondoka WCB hata kabla sijajiunga, kama ingetegemea mambo mengine ningesaini mkataba," alisema Zuchu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live