Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zuchu aikacha bethidei ya Diamond, ampa mashavu Mbosso

Zuchu Aikacha Bethidei Ya Diamond, Ampa Mashavu Mbosso Zuchu aikacha bethidei ya Diamond, ampa mashavu Mbosso

Wed, 4 Oct 2023 Chanzo: Tannzania

Malkia wa Bongo Fleva, Zuhura Othman almaarufu Zuchu mnamo siku ya Jumanne alisherehekea siku ya kuzaliwa msanii mwenzake katika WCB, Mbosso Khan.

Mbosso aliadhimisha siku yake ya kuzaliwa ya 31 Oktoba 3, siku moja tu baada ya bosi wake Diamond Platnumz kusherehekea siku yake ya kuzaliwa na ya mwanawe, Naseeb Jr.

Wakati wa kumsherehekea, Zuchu alionesha upendo kwa mwanabendi huyo wa zamani wa Yamoto Band kwa kumtakia heri ya siku ya kuzaliwa.

“Mshedada Khan @mbosso. Happy nepi day kaka,” Zuchu alimsherehekea Mbosso kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Mwimbaji huyo wa kibao ‘Sukari’ aliambatanisha ujumbe wake na picha ya Mbosso.

Ingawa Zuchu kumsherehekea Mbosso huenda ikaonekana ni jambo la kawaida tu, ishu ni kwamba malkia huyo wa Bongo Fleva hakumsherehekea hadharani bosi wake Diamond Platnumz ambaye pia anadaiwa kuwa mpenzi wake ilhali siku yake ya kuzaliwa ilikuwa siku moja tu kabla, Oktoba 2.

Zuchu hakuweka post yoyote kwenye mtandao wa kijamii akimtakia heri ya siku ya kuzaliwa bosi huyo wa WCB siku ya Jumatatu ilhali watu wengine wengi walimsherehekea.

Haijabainika iwapo hatua hiyo ilifanywa kimakusudi au alimsherehekea kwa njia nyingine.

Haya yanajiri siku chache tu baada ya malkia huyo kutoka Zanzibar kudaiwa kugombana na mama ya Diamond, Sanura Kassim almaarufu Mama Dangote kuhusu aliyekuwa mpenzi wa mwimbaji huyo na ambaye ni mzazi mwenzake, Tanasha Donna.

Tetesi za mzozo kati ya Mama Dangote na Zuchu ziliibuka wiki jana baada ya mama huyo wa Diamond kudaiwa kum-unfollow malkia huyo wa bongofleva kwenye Instagram. Pia alidaiwa kukubaliana na maoni ya shabiki mmoja aliyependekeza Diamond kurudiana na Tanasha na kumtimua Zuchu.

Wakati akijibu tuhuma hizo, Mama Dangote aliweka wazi kuwa hajamfuata wala kum-unfollow mtu yeyote kwenye Instagram hivi majuzi.

“Mimi wasije wakaniingiza kwenye mambo yao. Mimi sijamu-unfollow. Niliowa-follow hao hamsini, ndio hao hao hamsini. Sasa nimuunfollow kwa kipi?” Mama Dangote aliiambia Wasafi Media.

Aliongeza, “Mimi mwenyewe ata nikigombana na mtu atajua mwenyewe. Niliowa-follow ni hao hamsini ,sina hamsini na moja. Mambo ya kitoto ya zamani wasiniingize. Mimi najijua mtu mzima. Mimi nimuunfollow amenifanya nini?”

Mama Diamond pia alikanusha madai ya ku-pin maoni ya mtumizi wa Instagram ambaye alidai kuwa Tanasha Donna ndiye mke sahihi wa bosi huyo wa WCB na kupendekeza kuwa ni wakati wa yeye kumtimua Zuchu na kumfanya awe kicheko.

“Wanasema eti mimi nime-pin comment. Ni nini? Simu ya iPhone sijui kutumia. Nimegusa labda kimakosa. Jana (Jumatano) simu sikuwa nayo, nilikuwa na wageni. Nimegusa saa ngapi? Kupost kwenyewe siposti. Kassim ndiye ananipostia, mimi siwezi nimepewa tu simu iPhone na Naseeb. Siwezi,” alisema Mama Dangote.

Mama mzazi wa staa huyo wa Bongo aliwasihi wanamitandao kuepuka kumuingiza kwenye ugomvi na Zuchu huku akimtaja malkia wa Zanzibar kama bintiye.

“Wasinigombanishe na mwanangu Zuchu. Mimi sina ugomvi na mtu. Wasiniingize kwenye mambo hayo,” alisema.

Chanzo: Tannzania