Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zuchu afunguka kuwa na mahusiano na Diamond

Zuchu Na Diamondyyy Zuchu afunguka kuwa na mahusiano na Diamond

Thu, 18 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kuzungumzwa mengi na vitendo kuonekana kwa mapichapicha mtandaoni, mtoto mzuri kutoka Wasafi Classic Baby (WCB), Zuhura Othuman Soud ‘Zuchu’ ameweka wazi kuhusu madai ya kutoka na bosi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

Zuchu amesema, Diamond ni bosi wake na amekuwa akisafiri naye nje ya nchi kama ambavyo wasanii wengine huwa wanasafiri na bosi wao huyo kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali.

“Simba anasafiri na wasanii wengi. Mimi nimeenda naye Paris ni kama msanii wake. Nimejifunza mengi, nimepata expirience. Hakuna zaidi ya urafiki,” anasema Zuchu. Alipoulizwa ni mwanaume gani anapenda awe mpenzi wake, Zuchu alisema hana taipu zaidi mtu awe mwema.

“Mimi sina taipu, mtu yeyote na aweza kuwa na mimi. Ili mradi tu wue mtu mwema kwangu. Mkarimu, mtu mzuri sana,” alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live