Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zuchu afunguka ishu ya WCB kunyonya wasanii!

Zuchu Na Mondiii.png Zuchu afunguka ishu ya WCB kunyonya wasanii!

Wed, 17 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Queen wa Bongo Fleva, Zuhura Othman Soud ‘Zuchu’ ameweka bayana kuwa, hajazingatia chochote kuhusu kelele za wasanii wanaodaiwa kunyonywa na lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB).

Amesema, suala hilo amelisikia kwenye mitandao lakini yeye anaona lipo kwa kila msanii na namna ambavyo aliingia mkataba na WCB hivyo kama akiona kuna kipengele hakipo sawa basi nafasi ipo ya kurekebisha kuliko kulalamika.

“Sikuwahi kuona mkataba wa msanii yeyote. Hivyo hata ikitokea unataka kuondoka ni maamuzi ya mtu binafsi. Kila mtu ana malengo yake. Siamini kila kinachozungumzwa na watu kwenye mitandao.

“Ninachofahamu kila mkataba una makubaliano. Kila kitu kanaweza kuzungumzika kama una malalamiko nadhani unaweza kuzungumza na mkaelewana,” anasema Zuchu na kuongeza.

“Mimi kama nina kipengele ambacho mimi labda sikipendi nina uwezo wa kuifata menejimenti nikawaomba tubadilishe na wakanisikiliza.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live