Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zuchu adaiwa kuanza kujichubua

Zuchu Klm Zuchu

Mon, 29 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zuchu; ni malkia mpya wa muziki wa Kizazi Kipya nchini Tanzania ambaye anadaiwa kuanza kujichubua.

Madai hayo ya kwenye mitandao ya kijamii yanasema kuwa, ustaa huja na mambo mengi ambapo kabla ya mtu kuwa staa huonekana katika uhalisia wake wa ngozi, lakini akishapata umaarufu huanza kujibadilisha kuanzia ngozi hadi maumbile.

Hata hivyo, katikati ya madai hayo, mama mzazi wa Zuchu ambaye ni mkongwe wa muziki wa Taarab, Bi Khadija Kopa ameingilia kati kumtetea bintiye.

Bi Khadija anasema kuwa, Zuchu amekuwa na ngozi nyeupe katika siku zote za maisha yake.

“Zuhura (Zuchu) hivyo alivyo yuko vile. Zuhura mweupe tangu alipozaliwa, yeye na kaka’ke, marehemu Omari. Watoto wangu walikuwa wawili weupe na wawili weusi,” anasema Bi Khadija.

Anasema kuwa, hakuna uwezekano kuwa Zuchu anajichumbua ngozi na kudai kuwa picha za mitandaoni zinazoonesha akiwa mweupe zaidi huwenda zimeeditiwa kwa kutumia kompyuta.

“Yuko vilevile alivyozaliwa. Ukiona picha kwenye simu labda imeeditiwa kwa kutumia filter. Lakini uso yuko vile. Rangi yake ile. Hajichubui,” anasema. Kumekuwa na tetesi kuwa Zuchu amekuwa akijaribu kujibadilisha tangu alipojizolea umaarufu mkubwa baada ya kujiunga na WCB.

Zuchu alisajiliwa na Diamond Platnumz kwenye lebo yake hiyo mwaka 2020 na umaarufu wake umeendelea kukua siku hadi siku.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live