Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zuchu: Nimemwambia Nandy aniandikie Dua

Zuchu Nandy M.jpeg Zuchu: Nimemwambia Nandy aniandikie Dua

Tue, 16 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Fleva kutoka Lebo ya Wasafi, Zuchu ameamua kufunguka sababu ya kutohudhuria harusi ya wasanii wenzake, Nandy na Billnass licha ya kupewa mwaliko.

Zuchu amesema siku ya harusi hiyo alikuwa na majukumu mengine ya kazi hivyo akashindwa kuhudhuria huku akionyesha pia kushangazwa na namna gani nandy ameweza kufunga ndoa ilihali ni msanii na akiwa na ujauzito.

"Mara ya mwisho nimezungumza naye ilikuwa siku ya harusi yake, aliniomba niende kwenye harusi yake lakini nilikua na vimeo nikamwambia sitoweza kuhudhuria lakini baada ya harusi yake nikampongeza nikamwambia ndugu yangu umeweza umeolewa? Nikamwambia wewe ni msanii wa kike hapo ulipo una mimba na umeolewa.

“So nikamwambia umewezaje? Niandikie tu dua yako niikeshee hiyo dua, nikamwambia niandike mpaka nukta nikipiga goti nijue ninachokiomba, akaniambia Zuchu na wewe utapata tu Mungu akijalia maana ndoa andazi kila mtu anaweza kununua? Nimempongeza na nimefurahi juu yake, lakini ukweli unaouma ni kwamba ukiwa msanii wa kike ndoa ni ndoto ambayo hutakiwi kuiwaza sana.

''Kwa upande wangu ni kitu ambacho nimeishi nacho kwenye maisha yangu, mama yangu ni mwanamke mzuri roho yake safi lakini unaona kabisa kama vile hujapangiwa ilo jambo, kwahiyoo kuna ile mtu kama #nandy akiolewa na bado anaendelea na muziki naona kumbe inawezekana,” amesema Zuchu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live