Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zuchu: Kuanzia leo sina mahusiano na Diamond

ZUCHU NA DIAMOND VIDEO MPYA Zuchu: Kuanzia leo sina mahusiano na Diamond

Fri, 23 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Fleva, Zuchu amesema kuwa kuanzia leo amevunja uhusiano wake na mpenzi wake Diamond Platnumz baada ya wawili hao kutofautiana.

Zuchu amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram ikiwa ni siku moja baada ya Diamond kupost picha akiwa na mzazi mwezake (ex wake), Zari The Boss Lady hapo jana, jambo ambalo linaonekana limemuudhi Zuchu.

"Helo fan-milly. I had to post this to clear my conscience. Kuanzia leo hii mimi na Nasibu (Diamond) hatuko pamoja. I know this has been our thing but as hard as it is kumuacha mtu unaempenda hii naomba mungu iwe ya mwisho na nianze maisha mapya.

"Mapenzi ni heshima kwa bahati mbaya sana hiko kimekosekana kwetu, as for him bado tuna kazi za pamoja i wish him and his family the absolute best. Tumeishi vizuri lakini nadhani hii sio rizki.

"Mwaka huu nimejifunza kusema hapana kwa kila kitu kisichonipa furaha ama baada ya kusema haya naona kabisa naenda kuanza ukurasa mpya wenye maisha yaliyojaa furaha, uhuru na amani. As for now kazi iendelee and I am single.

Yours truly Zuchu."

View this post on Instagram

A post shared by ZUCHU (@officialzuchu)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live