Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zuchu: Diamond ndiye amenitoa usichana wangu

Zuchu Diamond Fsrss Zuchu: Diamond ndiye amenitoa usichana wangu

Mon, 11 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii malkia wa Bongo Fleva Zuchu amethibitisha bayana kwamba bosi wake ambaye pia ndio mpenzi wake Diamond Platnumz ndoye mwanamume wa kwanza kushiriki kimapenzi.

Katika kile kiichoonekana kama ni kipindi cha maswali na majibu na mtangazaji wa Wasafi, walikuwa wamepewa vijikaratasi vilivyokunjwa na ambavyo ndani mwao kulikuwa kumeandikwa maswali kwa ajili yao kujibu.

Katika moja ya swali, Zuchu aliulizwa kujibu mpaka sasa ni wanaume wangapi ambao ameshatoka nao kimapenzi.

“Mpaka sasa ni wanaume au wanawake wangapi umeshawahi kulala nao kimapenzi,” swali liliuliza kwa mshangao wa Zuchu.

“Ni mmoja tu, Diamond Platnumz ndiye mwanaume wangu wa kwanza kuwa naye kwenye mahusiano, sikuwahi kuwa kwenye mahusiano tangu nizaliwe. Mwanaume wangu yupi mwingine unayemjua ndani ya tasnia au nje ya tasnia?," Zuchu alijibu.

Kisha alimrukia na kumkumbatia Diamond ambaye walikuwa naye kwenye mlango wa chumba chao walimokuwa wamefikia huku naye bosi huyo wa Wasafi akionekana kutojiweza kwa jinsi Zuchu alikuwa anampunga kwa mapenzi mubashara.

Kwa kile kilichooneaka kama ni kushangaza kwa wengi, Zuchu aliwataka watangazaji hao pia kumuuliza swali hilo Diamond.

Diamond tena bila aibu alijibu kwamba hajawahi tembea na mwanamke mwingine kimapenzi Zaidi ya Zuchu tu.

Diamond alijibu hili licha ya kujulikana wazi tena na kila mtu kwamba ameshatoka kimapenzi na wanawake wengi tena wenye hadhi za juu akiwemo Wema Sepetu, Hamisa Mobetto, Zari Hassan, Tanasha Dona na wengine baadhi tu kwa kutaja.

Zaidi ya hapo, Diamond tayari ni baba kwa watoto wengi, akiwa na wawili na Zari, mmoja na Tanasha na mmoja na Hamisa Mobetto.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live