Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zuchu, Diamond kimeeleweka baada ya mwamba kupiga goti

Diamond Na Zuchu HJ.jpeg Zuchu, Diamond kimeeleweka baada ya mwamba kupiga goti

Mon, 26 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bifu ya mapenzi kati ya Mastaa wa Bongo fleva Zuhura Othumani 'Zuchu' @officialzuchu na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz' imeisha kwa sasa baada ya Platnumz ‘kupiga goti’ jukwaani wakati Zuchu akitumbwiza kwenye Full Moon Party iliyokuwa ikifanyika Kendwa Rocks Hotel mjini Zanzibar.

Akiomba msamaha, Platnumz @diamondplatnumz's amesema baada ya mazungumzo na Zuchu sasa wanawake wengine atawaona kama dada zake.

Zuchu amedai kuwa alikuwa akiteseka kwa karibu miezi 6 na ilibidi afiche machungu yake kwa kuvaa sura ya tabasamu. “Naonyesha mwenyewe furaha lakini moyoni kuna mengi nayapitia hamjui,” amesema Zuchu.

Mtunzi huyo wa “Honey” anasema hakuwa sawa sio tu kwa sababu ya mapenzi, “hata maisha kwa ujumla.” Ameongeza kuwa kwa maneno ya mitandaoni anafahamu wachache wanampenda na wengi wanamchukia.

Mapema jana, Zarina Hassan @ZariTheBossLady ama Mama T ambaye ni Mama Watoto wa Mwimbaji Diamond Platnumz, aliiambia AyoTV kuwa alikuwa hahusiki na mgogoro wa kimapenzi kati ya Platnumz na Zuchu.

Mama T alitajwa kuwa pengine anaweza kuwa chanzo cha mgogoro wao baada ya Platinumz kuchapisha video wakiwa wameshikana na Mama T. Hatahivyo (Mama T) amesema alifanya hivyo kwa kuwa Platnumz aliomba msaada “support” kuchagiza video ya wimbo wake mpya “Mapozi” aliowashirikisha Herry Sameer @mrbluebyser1988 na Jaymelody @realjaymelody

Chanzo: www.tanzaniaweb.live