Binadamu ana viungo kadhaa ambavyo vinaweza kumtambulisha kuhusu afya yake na mojawapo ni ngozi, macho na kucha ambazo zinatambulisha mengi kwa kuzingatia mabadiliko ya rangi.
Tukiangalia macho yakiwa ya bluu tangu kuzaliwa ni utambulisho wa kuwapo na ualbino. Wakati ngozi ikiwa ya njano ni dalili za homa ya jondizi hata matatizo ya ini.
Kadhalika kucha nazo zinaelezea afya yako na kinaweza kuwa kipimo tosha cha kuuchunguza menendo wa hali ya mwili, inaripoti makala ya BBC.
Inataja sehemu hii ya mwili kuwa inaweza kuonyesha matatizo mbalimbali ya afya yanayobainishwa na mabadiliko ya rangi, kwenye kucha na vipengele vingine vinavyotumika kama tahadhari kwa magonjwa.
Hii inapotokea, inashauriwa kutafuta daktari wa ngozi ili kutathmini kwa kina na kufanya vipimo kama vile vya damu na daktari anaweza kuamua.
Wakati akishuku kunaweza kuwa na tatizo kubwa mtaalamu wa afya anaweza kuagiza seli au tishu kuchunguzwa zaidi.
Matatizo ya kawaida husababishwa na figo, ngozi, ini, lishe, na hali ambayo mfumo wa kinga ya mwili hushambulia seli zenye afya au autoimmune.
Habari njema ni kwamba tofauti fulani za kucha hazimaanishi shida kubwa kila wakati, mara nyingi husababishwa na utaratibu wa urembo.
"Kucha za miguuni hazitunzwi sana na wakati mwingine zinakabiliwa na matatizo zaidi. Kucha kwa mfano, inaweza kuwa ya njano na nzito," anasema Valéria Zanela Franzon, daktari wa ngozi na profesa wa tiba katika Chuo Kikuu cha Katoliki huko Paraná.
KUASHIRIA MATATIZO
Zifuatazo ni ishara kadhaa ambazo zinaweza kuonyesha matatizo ya kiafya na zinastahili kuchunguzwa:
KUCHA NYEUPE
Rangi nyeupe, doa jepesi linaweza kuashiria ugonjwa wa mycosis, ni maradhi yanayosababishwa na kuvu au fangasi kwenye ngozi au kucha. Mycosis inaosababishwa na kuambukizwa na vimelea, kama vile upele. Au maradhi yaitwayo psoriasis ambao ni ni upele kwenye ngozi, lakini wakati mwingine ukihusisha kucha na viungo.
Ugonjwa wa ngozi unaosababisha vipele vinavyowasha, mabaka, magamba, mara nyingi kwenye magoti, viwiko, shina na ngozi ya kichwa na nimonia au homa ya mapafu na hata moyo kushindwa kufanya kazi vizuri.
Ukosefu wa baadhi ya virutubisho, utapiamlo na chakula kukosa protini pia husababisha kuwa na kucha nyeupe.
Aidha kunaweza pia kuonyesha upungufu wa damu pia, husababishwa na ukosefu wa madini ya chuma na kunaweza kufanya ukucha uwe na umbo la kijiko na kukunjamana," asema Juliana Piquet, daktari wa ngozi na mshiriki wa Jumuiya ya Madaktari ya Ngozi ya Brazil na Jumuiya ya Amerika kwa Tiba ya Laza na Upasuaji.
Pia anataja ‘leukonychia’, ni madoa meupe kwenye kucha, akisema kwa kawaida si ishara ya kutisha, lakini wakati mwingine inaweza kufichua matatizo makubwa ya utaratibu au hali ya kuzaliwa.
Ili kutibu hali hizi, madaktari huwaomba mgonjwa kuchunguza sababu ya tatizo. Kwa hiyo, unashauriwa kufanya vipimo mbalimbali na ufuatiliaji na mtaalamu wa ngozi na wataalamu wengine wa masuala ya moyo na lishe.
KUCHA YA NJANO
Rangi hii inaweza kuwa na sifa ya urithi wa maumbile au kwa kuzeeka kwa kucha na kuwa nyepesi na kwa rangi ya njano.
Inaweza pia kutokana na rangi inayosababishwa na mycoses au fungasi.
Katika hali mbaya zaidi, pia inaonyesha hali kama vile kuwapo kwa Virusi Vya UKIMWI na ugonjwa wa figo.
Wavutaji sigara wanaweza pia kubadilisha rangi ya kucha zao, kutokana na kushika sigara moja kwa moja. Rangi hii kawaida huonekana kwenye kucha ya kidole kinachoshika sigara.
MABAKA MEUPE
Mabaka haya yanajulikana kama ‘pitting dots’ na zinaweza kuonekana kwenye kucha.
Yanahusishwa na ugonjwa wa ngozi unaojulikana kama atopic dermatitis -hali ambayo husababisha ngozi kuwa kavu, kuwasha na kuvimba na hali nyingine za ngozi na nywele.
Ni kawaida kwa watoto wadogo, lakini inaweza kutokea katika umri wowote. Mabaka haya yanahusishwa na ugonjwa wa ngozi unaojulikana kama atopic dermatitis.
BLUU
Ingawa ni nadra kuwa na kucha za bluu lakini rangi hii inaweza kutokana na matumizi ya dawa maalum. Mojawapo ya kawaida ni zile zinazotibu chunusi na dawa za malaria. Wakati hali hii inapojitokeza, daktari lazima atathmini ikiwa kuna haja ya kusimamisha dawa fulani na kuendelea na aina mpya ya matibabu.
"Inazingatiwa ikiwa kucha ndio udhihirisho pekee na athari ya pili inayokubalika," anaongeza Valéria Zanela Franzon.
Kucha yenye maambukizi ya mara kwa mara ya vimelea fangasi. Ni ugonjwa wa mycosis unasababishwa na maambukizi ya vimelea na unaweza kutokea tena wakati matibabu yanapositishwa.
Kama matibabu hayafanyiki vizuri, vimelea vinaweza kutokea na kushambulia kucha mara kwa mara hata kusababisha kuonekana kama zimekufa au kuoza.
Tatizo linaathiri zaidi kucha miguuni na linapaswa kutibiwa hadi miezi sita.
Katika mikono inashauriwa kutibu kwa muda wa miezi mitatu hadi minne.
Mwathiriwa anapaswa kuzingatia masharti na na wakati unaofaa wa kila dawa na kufuata kwa makini ushauri wa daktari hadi matibabu yatakapokamilika.
KUWAPO MISTARI
Kitaalamu inajulikana kama mistari ya ‘beau’, inafanana na mistari ya wima au kulala na inaweza kuonekana baada ya homa kali au matibabu maalum na kuacha kucha zikiwa na makunyanzi zaidi.
Wakati mistari inapokuwa kama meusi au ya kahawia au giza na kuonekana kwenye kidole kimoja tu, inaashiria hali inayofahamika kama melanoma, ambayo ni saratani ya kucha au ya ngozi.
Hata hivyo ukweli unafahamika kwa kwenda hospitalini siyo kuona dalili bila kufanyiwa uchunguzi wa kitaalamu.