Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ziara ya Tylor Swift yaongoza kwa maokoto, yaweka rekodi Guinness

Ziara Ya Tylor Swift Yaongoza Kwa Maokoto, Yaweka Rekodi Guinness Ziara ya Tylor Swift yaongoza kwa maokoto, yaweka rekodi Guinness

Wed, 13 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki kutoka nchini Marekani Taylor Swift kwa sasa ndiye anayepata pesa nyingi katika show za muziki ambapo ziara yake ‘The Eras Tour’ imeingia kwenye Kitabu cha Kumbukumbu za dunia ‘Guinness World Records’ kwa kuwa ziara iliyoingiza pesa ndefu zaidi kwa muda wote.

Ziara hiyo imeingiza kiasi cha dola 1.04 bilioni zaidi ya tsh. 2.5 trilioni kwenye matamasha 60 ambayo ameyafanya hadi sasa kwenye maeneo mbalimbali dunia.

Pia ziara hiyo ina jumla ya maonesho 151 hivyo bado maonesho 91 kukamilisha mzunguko wote ambao ulianza March 17, 2023 na utamalizika Disemba 8, 2024.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live