Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zari kuolewa tena ndoa ya tatu

Zari 7 Zari kuolewa tena ndoa ya tatu

Mon, 14 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zari The Boss Lady @zarithebosslady ; ni mwanamama tajiri Afrika Mashariki na baby mama wa staa mkubwa wa muziki nchini Tanzania, Diamond Platnumz ambaye anaendelea kula bata na mpenzi wake na kupelekea kuacha misonyo kama yote.

Zari ambaye ni raia wa nchini Uganda mwenye maskani yake pale Durban nchini Afrika Kusini alikataa kufichua jina la mpenzi wake huyo wakati alipoombwa kufanya vile, lakini Gazeti moja kubwa nchini Tanzania linamjua kuwa ni kutoka mkoani Iringa, ila anaishi nchini Afrika Kusini.

Hatua hiyo ya Zari kumtambulisha mpenzi mpya inajiri baada ya kuachana na mfanyibiashara wa Uganda miezi miwili iliyopita aitwaye GK Choppa.

Waja wamegundua kwamba, Zari amevunja mahusiano yake na GK Choppa pale alipofuta picha zao zote kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Mahusiano ya Zari na mfanyibiashara huyo yalizua utata mitandaoni kwani alionekana kuwa mwenye umri mdogo kuliko.

Mama huyo wa watoto watano anadaiwa kupendelea kujitosa kwenye mahusiano na wanaume wenye umri mdogo kuliko yeye.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live