Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zari anataka mtoto wa sita

Zarii Sdg Zari anataka mtoto wa sita

Mon, 19 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanasosholaiti na mjasiriamali maarufu Afrika Mashariki, Zari Hassan ametangaza kuwa ananuwia kupata mtoto wa sita na mumewe Shakib Lutaaya.

Zari kupitia ujumbe wake kwa bwanake siku ya kusherehekea wazazi wa kiume, alisema kuwa anapanga kumfanya mumewe baba wa watoto wawili.

Alikosa kumsherehekea baba ya watoto wake wawili, mwanamuziki Diamond Platnumz.

“Heri za siku ya kina baba duniani mpenzi wangu. Sasa wewe ni baba ya mtoto 1 ninatumai uwe baba ya watoto wawili Inshaallah,” akaandika.

Tayari, Zari ana watoto tano, watatu ambao aliwapata na mwanabiashara Ivan Ssemwanga ambaye aliaga dunia mnamo 2017.

Zari na Shakib walifunga ndoa Aprili 2023 japo katika hafla ya faragha.

Disemba mwaka jana, 2023, Shakib alimpeleka Zari kwa wazazi wake kuonyesha anawajibikia uhusiano wao.

Japo wamewachana kwa miaka 12 kiumri, wanandoa hao wamepuuza dhihaki za watu mitandaoni.

“Shakib si mtoto. Ni mtu mzima wa kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi nami. Nina umri wa miaka 42 naye 30. Shida iko wapi? Kuna wanaume wengi ambao huoa wasichana ambao hawajatimia miaka ya ndoa na hawapingwi. Kwa hivyo sifanyi kosa lolote,” akajitetea.

Mwezi Mei 2023, Zari alitangaza kuwa atafunga ndoa tena mwaka huu.

“Harusi yetu ilikuwa kichinichini na ilifanyika tu vile tulivyopanga. Inshallah tutafanya harusi nyingine kabla mwaka huu kuisha. Tumechagua kuifanyia Uganda sababu huko ndiko wanafamilia wetu wapo,” akasema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live