Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zari amaliza utata ukaribu wake na Diamond

Zari Amaliza Utata Ukaribu Wake Na Diamond Zari amaliza utata ukaribu wake na Diamond

Mon, 18 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa Zari The BossLady amefunguka juu ya ukaribu wake wa sasa na mzazi mwenzie, staa wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz.

Hivi karibuni tumeona familia za wawili hao zikiwa karibu tofauti na mwanzao, Zari amedai kuwa yeye na Staa huyo kabla hawajawa na mahusiano ya kimapenzi walikuwa marafiki wa karibu na hawakuachana na kwa ubaya ndio maana imekuwa rahisi wao kuwa na ukaribu walio nao kwa sasa.

"Hatujawahi kuwa na ubaya kati yetu mnavyotuona karibu sio kama tumerudiana, yeye ni rafiki yangu, tunazungumza, ni baba wa watoto wangu, naweza kumpigia simu na anaweza kuniita kwa kitu, hatukuachana na kwa ubaya," alisema Zari.

Wawili hao waliachana Mwaka 2018 baada ya kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi kwa miaka minne.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live