Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zari aipeleka familia yake Dubai kula bata, gharama ya hoteli waliyofikia ni moto (Picha/video)

5587 29094369 158987321437352 849734257034133504 N

Sun, 1 Apr 2018 Chanzo: bongo5.com

Zari The Boss Lady ametua nchini Dubai kwa ajili ya kula bata na kufurahia wikiendi ikiwa ni siku chache zimepita tangu aliposaini dili la mamilioni ya fedha na kampuni moja ya nepi za watato hapa Bongo.



Kupitia mtandao wa Instagram, mrembo huyo ameweka picha kadhaa akionyesha akiwa ameongozana na watoto wake wawili akiwemo Raphael G na Lil Q na mtu mwengine ambaye kwenye mtandao huo anatumia jina la @tingdis.

“Weekend mode activated….,” ameandika Zari kwenye moja ya picha alizoziweka Instagram.



Zari na familia yake hiyo wamefikia kwenye moja ya hoteli maarufu Dubai inayofahamika kama Dusit Residence Dubai Marina. Gharama za Kulala kwenye hoteli hiyo kwa usiku mmoja kwa bei ya chini ni takribani 385,000 hadi 1,010,000.

Hata hivyo inadaiwa kuwa ex huyo wa Diamond hivi karibuni atarudi tena Tanzania kwa ajili ya kusaini mkataba mwingine na kampuni ambayo bado haijafahamika.





Chanzo: bongo5.com