Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zari ahama jumba la Diamond Afrika Kusini

81577 Zaripic Zari ahama jumba la Diamond Afrika Kusini

Thu, 24 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Baada ya kusimangwa kwa muda mrefu na watu mbalimbali katika mitandao ya kijami, hatimaye Zarina Hassan, maarufu kwa jina la Zari The Bosslady ameondoka katika mjengo wa nyota wa muziki Tanzania, Diamond platnumz  baada ya kutishiwa kuwa nyumba hiyo ingeuzwa wakati akiwa ndani pamoja na watoto wake.

Zari amehamia sehemu nyingine kutoka katika jengo hilo la Diamond lililopo jijini Pretoria, Afrika Kusini, kwa mujibu wa tovuti ya ugandaonline.net. Pamoja na kutengana, Diamond alikuwa amemuuachia Zari aishi katika nyumba hiyo pamoja na familia yake—inayoundwa na watoto watatu aliozaa na mume wake wa zamani marehemu, Ivan na wawili (Latifa na Nillan) wa nyota huyo wa Boingofleva.

Zari amenunua mjengo huo katika siku ya kusherekea kutimiza miaka 39 tangu kuzaliwa kwake ambapo baada ya kununua nyumba hiyo alikarabati nje na ndani na kuipa muonekano mpya na wa kisasa zaidi.

Ikumbukwe kuwa Diamond alimnunulia Zari nyumba yake ya awali katika siku ya kusherekea siku yake ya kuzaliwa alipotimiza miaka 36. Wawili hao walikuwa wakiishi pamoja nchini Afrika Kusini na Tanzania. 

Chanzo: mwananchi.co.tz