Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zari afunguka mazito: Ningepigwa risasi kwa ajili ya Diamond

Diamond Zariii Diamond na familia yake.

Sat, 26 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zari alisema anafahamu baba ya watoto wake wawili Diamond alikuwa anatoka nje ya ndoa lakini aliamua kuyafumbia macho.

"Hata nyakati ambazo nilijua umekosea, ningenyamaza tu kwa ajili ya amani, tufurahie, tuyaache yaende, tusonge mbele, tuendelee na kuweka familia..."

Mama huyo wa watoto watano aliongeza kuwa angelalamikia tabia zake mbaya kila wakati, lakini Diamond mwenyewe hakushughulika.

"Ningekubali kupigwa risasi kwa ajili yako, lakini kila nilipokufanyia hivyo, ulifanya kinyume, mimi na watoto wako tulikuwa tukivamiwa, sikuwa na mahali pa kujificha," alisema.

Zari alikatiza mahusiano yao baada ya Diamond  kumpa ujauzito Hamisa Mobetto na hiyo ilikuwa thibitisho kuwa hakuwa mwaminifu.

"Watu hao wakioanza kutoa risiti za tabia zako, ulichofanya, na risiti ziko mbele ya macho yetu, mimi hujiondoa na kusema ndio, alifanya hivyo."

Kwa sasa Zari anatoka kimapenzi na bwenyenye wa Uganda anayetambulika kwa jina la GK Choppa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live