Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zari acharuka kisa kibenteni

Zari 7 Zari acharuka kisa kibenteni

Mon, 1 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mfanyabiashara maarufu kutoka Uganda, Zari The Bosslady amevunja ukimya na kuwajibu watu ambao wamekuwa wakimkosoa kwa kuwa na mahusiano na mwanaume mwenye umri mdogo kuliko yeye.

Akizungumza kwenye video ambayo aliiposti Insta Story, Zari alionekana kughadhabishwa sana na kusema ana haki ya kumchagua yule ambaye angependa kuwa naye.

"Niko hapa kwa sababu nataka kuwa hapa, sio kwa sababu mnataka kunichagulia mahali pa kuwa," alisema Zari.

Utakumbuka Zari ambaye ni mama wa watoto watano, hayo ni mahusiano yake ya kwanza kuyaweka wazi zaidi tangu kuachana na Diamond Platnumz mapema mwaka 2018.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live